HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 22, 2023

TACOGA 1984 YAWAPIGA MSASA WASHAURI, WANAFUNZI KUHUSU NAMNA BORA YA KUKUZA UTENDAJI WAO

Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida, Dk.James Mrema (katikati waliokaa), ambaye alimuwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Taasisi hiyo, Tanzania, Profesa William Pallangyo akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chama cha Ushauri na Uelekezi kwa Washauri wa Wanafunzi Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TACOGA 1984), baada ya kufungua mafunzo yanayohusu namna bora ya kukuza utendaji katika kuwapa ushauri wanafunzi wanao walea na kuwaongoza yalioanza Juni, 21, 2023. Kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti TACOGA 1984, Augustine Matemu, Mwenyekiti wa TACOGA 1984, Sophia Nchimbi,Mshauri wa Wanafunzi ISW na Katibu wa TACOGA 1984, Dk.Andrew Caleb Randa, Mshauri wa Wanafunzi Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU) na Naibu Katibu Mkuu wa TACOGA 1984, Mhandisi Saad Hassan

....................................................

Na Dotto Mwaibale, Singida

CHAMA cha Ushauri na Uelekezi kwa Washauri wa Wanafunzi Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TACOGA 1984) kimewakutanisha washauri wa wanafunzi kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu, Vyuo vya Kati, Vyuo vya Ufundi na viongozi wa Serikali za Wanafunzi.

TACOGA 1984 imewakutanisha wadau hao kwa ajili ya kuwawezesha kupata mafunzo yanayohusu namna bora ya kukuza utendaji katika kuwapa ushauri wanafunzi wanao walea na kuwaongoza.

Akifungua mafunzo hayo Juni 21, 2023 kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Mkurugenzi wa TIA Kampasi ya Singida, Dk.James Mrema aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kujikita zaidi katika changamoto zinazo likabili Taifa hasa suala la malezi ya vijana kutokana na utandawazi. 

Dk.Mrema alisema mmomonyoko wa maadili kwa vijana ni changamoto katika jamii ya watanzania na unarudisha nyuma maendeleo ya Taifa hivyo ni muhimu mafunzo hayo yalenge kupanga mbinu za kuwalinda vjana.

Ifahamike kuwa kasi ya kuporomoka kwa maadili inachochewa na ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano ambapo watoto na vijana wanaiga tamaduni na desturi za jamii zingine zinazo kinzana na mila za mtanzania hivyo hatua za haraka zisipochukuliwa hali itazidi kuwa mbaya zaidi,” alisema Mrema.

Dk. Mrema alitoa rai kwa washiriki wa mafunzo hayo wayatumie kama chachu ya kuwawezesha kupata mbinu bora zaidi katika kutatua changamoto za mmomonyoko wa maadili kwa vijana wa taifa la Tanzania. 

Alisema ni matumaini yake kuwa pamoja na kupata mafunzo hayo ya siku tatu, yatakayotolewa na wataalam tofauti tofauti , pia watapata fursa ya kujadili na kubaini changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa jukumu lao la kutoa ushauri kwa wanafunzi wa vyuo hivyo na kuwa mijadala hiyo itafanyika kwa lengo la kuibua mbinu bora za kukabiliana na changamoto hizo, ili waweze kuboresha na kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Aidha, Mrema alitumia nafasi hiyo kutoa pongezi zake za dhati kwa Kamati Tendaji ya TACOGA 1984, kwa maandalizi mazuri pamoja na  kwa washiriki wote kwa kuitikia wito wa kuhudhuria mafunzo hayo.

Mwenyekitiwa TACOGA1984, Sophia Nchimbi, alisema kazi kubwa wanayoifanya ni kutoa ushauri nasihi kwa wanafunzi na kwa wafanyakazi, kutoa mafunzo kwa Serikali za wanafunzi na kwa sekondari kuhusu mambo mbalimbali ya nasihi na kwa wadau wengine. 

Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Augustine Matemu alisema chama hicho kina malengo makubwa moja ya malengo hayo ni kuwajengea uwezo wa washauri wa wanafunzi na wafanyakazi wote waliopo kwenye ofisi ya ushauri.

Alitaja lengo lingine kuwa ni kukifanya kuwa ni chama cha watu waliobobea kwa kutengeneza bodi kama walivyofanya wahasibu, watu wa manunuzi na watu wa rasilimali watu.

Alisema kutokana na teknolojia kukua na mambo ya watu kuwa mengi wameona chama hicho kiwe cha kitaaluma zaidi jambo litakalowasaidia vijana ambao wanakabiliwa na changamoto nyingi.

Mlezi wa Wanafunziwa Chuo Kikuu cha Zanzibar, Mhandisi Saad Hassan  ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa TACOGA 1984, alisema chama hicho kipo katika vyuo vikuu vyote vilivyopo Zanzibar na kuwa wanachama wamekuwa wakishirikiana vizuri katika pande zote za Muungano yaani Tanzania Bara na Zanzibar.

Kwa upande wake Mratibu wa madawati ya jinsia wa vyuo vikuu na vyuo vya kati kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, Gift Msohoya alisema wizara imeandaa madawati ya jinsia vyuoni kutokana na agizo la Rais Samia Suluhu Hassan ili kuviwezesha kukabiliana na ukatili wa aina zote na kuwa watendaji wanayosimamia madawati hayo tayari wapo kazini.

Alisema hadi sasa vyuo 290 hapa nchini tayari vimekwisha anzisha madawati hayo na lengo ni vyote viwe nayo.

Mshauri wa Wanafunzi kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, Ukende Mkumbo, alisema chuo hicho kimekuwa mwanachama hai wa TACOGA 1984 tangu kianzishwe mwaka 1984.

Alisema TACOGA 1984 imekuwa msaada mkubwa kwa vyuo kwani imekuwa ikiwanoa washauri wote wa wanafunzi kwa ngazi zote kwa kuwapa semina, maarifa na mbinu ambazo zitawasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikumba jamii na wanafunzi.

“TACOGA 1984 imepewa kazi na Serikali ya kuhakikisha inawanoa vijana hawa kitaaluma watoke kama wataalam wanaoweza kujitosheleza na kujenga nchi na kuwa na mazingira mazuri ya kusomea na kuwasaidia wanaondokana na changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kuwafanya wakatishe masomo yao,”alisema Mkumbo.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida, Dk.James Mrema, akifungua mafunzo hayo. Kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti TACOGA 1984, Augustine Matemu, Mwenyekiti wa TACOGA, Sophia Nchimbi,Mshauri wa Wanafunzi ISW na Katibu wa TACOGA 1984, Dk.Andrew Caleb Randa, Mshauri wa Wanafunzi Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU) na Naibu Katibu Mkuu wa TACOGA 1984, Mhandisi Saad Hassan

Mwenyekitiwa TACOGA 1984, Sophia Nchimbi, akitoa taarifa kuhusu chama hicho.
Mratibu wa madawati wa vyuo vikuu na vyuo vya kati kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, Gift Msohoya, akizungumzia uanzishwaji wa madawati ya kijinsia katika vyuo.
Mshauri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ally Sanga, akitoa mada kuhusu Afya ya Akili.
Mshauri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salam (UDSM), Subira Mollel, akijibu maswali kuhusu Afya ya Akili.
Naibu Mshauri wa Wanafunzi MUDCC na Katibu Mwenezi wa TACOGA 1984, Zitta Victoria Mnyanyi. akizungumza kwenye mafunzo hayo
Mkurugenzi wa Huduma za Wanafunzi kutoka Chuo cha Ushirika Moshi,Dk.Elifisa Nnko akichangia jambo wakati wa mafunzo hayo.
Mkuu wa Idara ya Ushauri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk.Bernadetha Rushahu, akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.

Picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja na Kamati Tendaji. Waliokaa kutoka kushoto ni  Mkuu wa Kitengo cha Ushauri Nasaha kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dk.Bernadetha Rushahu, Makamu Mwenyekiti TACOGA 1984, Augustine Matemu, Mwenyekiti wa TACOGA, Sophia Nchimbi, Mratibu wa Dawati la Jinsia (MOCDGWS) Gift Msohoya na Mtoa Ushauri Nasaha kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ally Sanga. Waliosimama kutoka kusoto ni Mshauru Nasaha kutoka MUHAS na Mhazini wa TACOGA, Ruth Kitundu, Mshauri wa Wanafunzi wa Chuo cha KCMUCo na Mjumbe wa TACOGA 1984, Anza-Amen Lema, Mshauri wa Wanafunzi ISW na Katibu wa TACOGA 1984, Dk.Andrew Caleb, Mshauri wa Wanafunzi Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU) na Naibu Katibu Mkuu wa TACOGA 1984, Mhandisi Saad Hassan na Naibu Mshauri wa Wanafunzi MUDCC na Katibu Mwenezi wa TACOGA 1984, Zitta Victoria Mnyanyi.
Picha ya pamoja.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Kamati Tendaji
Taarifa kuhusu TACOGA 1984 ikitolewa.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo
Mafunzo yakiendelea.
Taswira ya mafunzo hayo.
 

No comments:

Post a Comment

Pages