Na Mwandishi Wetu
CHUO Kikuu Mzumbe wametangaza ongezeko la kozi mpya tatu ambazo zitafundishwa katika Chuo hicho, hayo yamesemwa na Mratibu wa Udahiri Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Michael Mangula.
Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam katika maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
"Niwataarifu kwamba Chuo Kikuu Mzumbe tuna programu zingine mpya ziko tatu ambazo zimeanzishwa na Chuo chetu, mbili ziko kwenye skuli ya Biashara ya utawala na menejimenti ambapo programu ya kwanza inaitwa 'Bachelor of Public Administration in Youth Development and Leadership'"Kozi hii imeazishwa mahususi ikiwa ni maagizo ya Serikali, sasa hivi tuwaandae wataalamu wanaosimamia maendeleo ya vijana kwa sababu vijana wakiwa na utaalamu haswa, ndio chanzo cha tija ya msingi kwa ajili ya kusimamia maendeleo.
"Kuna kozi nyingine inaitwa 'Bachelor of Health System in montary and evaluation' yenyewe inawaandaa wataalamu ambao wanasimamia miradi kwenye sekta ya afya, Ili kuendeleza miradi mingi sekta ya afya iwe endelevu." Amesema Dkt. Mangula na kuongeza kuwa.
"Kozi nyingine inaitwa 'Bachelor of Environmental Management' yenyewe inawaandaa wataalamu kwa ajili ya kusimamia shughuli za mazingira, tunaona kabisa sasa hivi kwenye viwanda au shughuli mbalimbali za uzalishaji zinafanyika lakini mazingira yamekuwa hayaangaliwi kwa kiasi kikubwa, kwaiyo tunaamini kwamba tukiandaa wataalamu watakuwa wanahakikisha kuwa shughuli za uzalishaji zinaendelea kwenye maeneo mbalimbali lakini zinazingatia suala la mazingira.
"Kwa maana ya kwamba tunakizi kizazi cha sasa bila kuathiri kizazi kinachokuja." Amesema Dkt. Mangula.
"Chuo Kikuu Mzumbe tuko hapa kwenye maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya kuwapa au kuwaelimisha wazazi, watoto na wananchi mbalimbali ambao wamemaliza kuanzia kidato cha nne, cha sita na diploma kwamba kama Chuo Kikuu Mzumbe tumefungua dirisha la udahiri kuanzia ngazi ya cheti, diploma, shahada za awali, shahada za umahili na shahada za uzamivu.
"Kama Chuo Kikuu Mzumbe sisi tunatoa mafunzo hayo ya muda mrefu kwenye maeneo mbalimbali ya ubobezi kwa upande wa Sheria, utawala na menejimenti, Biashara, Ujasiriamali, uhasibu na fedha, uchumi, tehama, takwimu tumizi, ualimu lakini pia kuna maeneo ya usimamizi wa shughuli za uzalishaji viwandani na shughuli ya kuwaandaa wahandisi wa kusimamia shughuli za uzalishaji kwenye viwanda." Dkt. Mangula amefafanua kuwa.
"Madirisha yako wazi, tumeyafungua, wakifika kwenye banda letu tunatambulisha programu ambazo tunazo kama Chuo Kikuu Mzumbe, tunawafahamisha ni programu zipi lakini pia tunawaelekeza sifa na namna ya kujiunga. Lakini pia mwanafunzi au mzazi atakayeelewa kuwa programu fulani sifa zake ni hizi itamsaidia kufanya maamuzi.
"Huduma nyingine tunayotoa ni kwamba tunafanya udahiri wa moja kwa moja, mwanafunzi akiwa na sifa hizo anafanyiwa udahiri hapa hapa mpaka tunamaliza, kwaiyo hana haja ya kutumia gharama nyingine za ziada kama mtandao, sisi wenyewe tunatoa hiyo huduma moja kwa moja."
"Nichukue tena nafasi hii kuwakaribisha wanafunzi, wazazi waliopo Dar es Salaam na mikoa jirani kutembelea Banda letu la Chuo Kikuu Mzumbe hapa viwanja vya Mnazi Mmoja kwa ajili ya kupata udahili wa moja kwa moja."amesema.
No comments:
Post a Comment