Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mobhare Matinyi (kulia), akizungumza na mjasiriamali kwenye banda mojawapo katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Julai 7, 2023 yanayoendelea kwenye viwanja vya SabaSaba Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.
DC Matinyi akiwa katika picha ya kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi wa Manisaa ya Temeke kwenye banda lao katika maonesho hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mobhare Matinyi akiwa katika picha ya kumbukumbu na baadhi ya wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 iliyotolewa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Na Khadija Kalili
MKUU wa Wilaya ya Temeke, Mobhare Matinyi, amepongeza ubora wa bidhaa za wajasiriamali waliowezeshwa kwa mikopo ya asilimia kumi na kuwataka waongeze uzalishaji ili wauze katika soko la kimataifa.
DC Matinyi amewashauri wajasiriamali waliowezeshwa kwa kupata mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, kuboresha bidhaa zao ili ziweze kuleta ushindani kwenye Soko la Kimataifa.
DC Matinyi amsema hayo leo Julai 7 2023 wakati alipotembelea mabanda ya wajasiriamali hao katika Maonesho ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya SabaSaba Dar es Salaam.
"Nimefurahi kuona wajasiriamali wakitumia fursa ya mikopo iliyotolewa na Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika juhudi za kupambana na tatizo la ajira lakini changamoto yetu kubwa siyo kwa Temeke tu bali nchi nzima ni namna ya kulipata soko la kimataifa. Tupambane hadi tufikie soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na lile la Afrika nzima kupitia Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Barani Afrika, amesema Matinyi.
Akijibu swali kuhusu tatizo la wananchi kuvamia maeneo ya wazi yanayomilikiwa na serikali, Mkuu wa Wilaya huyo ametoa wito kwa Idara ya Ardhi kuwaelimisha wananchi mara kwa mara na hata kuweka matangazo ili maeneo hayo yajulikane na kuepuka watu kuyavamia.
No comments:
Post a Comment