HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 08, 2023

Tanzania na Malawi kushirkiana kwenye Teknolojia ya Habari na Mawasiliano


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Malawi Mhe. Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera wakati wakishuhudia utiaji Saini Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya Tanzania na Malawi kuhusiana na mashirikiano kwenye Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) mara baada ya mazungumzo yao Lilongwe nchini Malawi tarehe 7 Julai, 2023. Aliyeketi (kulia) ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye wakisaini Mkataba huo pamoja na Waziri wa Habari na TEHAMA wa Malawi Mhe. Moses Kunkuyu Kalongashwa wa kwanza (kushoto).


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Malawi Mhe. Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera kwenye picha ya kumbukumbu na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye pamoja na Waziri wa Habari na TEHMA wa Malawi Mhe. Moses Kunkuyu Kalongashwa mara baada ya kushuhudia utiaji saini Mkataba wa Makubaliano (MoU) kuhusiana na mashirikiano kwenye Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Lilongwe nchini Malawi tarehe 7 Julai, 2023.

No comments:

Post a Comment

Pages