Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Temeke, Kidawa Masoud (wa pili kulia) akimkabidhi zawadi ya Runinga mfanyabiashara wa Kariakoo, Jackson Mbilinyi, wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa Promosheni ya mwisho ya Bonge la Mpango - Moto ni Uleule iliyofanyika kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam Julai 7, 2023. Wengine wakishuhudia ni wafanyakazi wa benki hiyo. (Na Mpiga Picha Wetu).
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper (kushoto) na Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Matawi wa Benki ya NMB, Donatus Richard (kulia), wakikabidhi kadi za pikipiki kwa washindi Sudi Rashid (wa pili kushoto) na Michael Mhando wa pili kulia) wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za Promosheni ya mwisho ya Bonge la Mpango - Moto ni Uleule iliyofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam Julai 7, 2023.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper, akimkabidhi zawadi ya mashine ya kufulia mshindi wa Promosheni ya Bonge la Mpango – Moto ni Uleule, Hamza Hamood Mohamed, katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika kwenye viwanja vya Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam Julai 7, 2023.
Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Matawi wa Benki ya NMB, Donatus Richard (wa pili kulia) akimkabidhi kadi ya Pikipiki ya magurudumu matatu (Guta), Hidaya Shomari, wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa Promosheni ya Bonge la Mpango – Moto ni Uleule. Kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper na kulia ni Meneja wa NMB Tawi la Temeke, Kidawa Masoud. (Na Mpiga Picha Wetu).Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Matawi wa Benki ya NMB, Donatus Richard (wa pili kulia) akimkabidhi kadi ya Pikipiki ya magurudumu matatu (Guta) mwakilishi wa wafanyabiashara kutoka mkoani Manyara, Yusuph Mbaya. Kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper na kulia ni Meneja wa NMB Tawi la Temeke, Kidawa Masoud.
Washindi wa Promosheni ya mwisho ya Bonge la Mpango - Moto ni Uleule, Sudi Rashid (wa pili kushoto) na Michael Mhando (wa pili kulia) wakiwa na furaha baada ya kukabidhiwa zawadi za pikipiki walizoshinda katika promosheni hiyo. Kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper na kulia ni Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Matawi wa Benki ya NMB, Donatus Richard.
Mkazi wa jijini Mwanza, Nande Tulimwanye, akionesha furaha yake baada ya kupokea zawadi ya Pikipiki ya magurudumu matatu (Guta) aliyojishindia katika Promosheni ya mwisho ya Bonge la Mpango - Moto ni Uleule iliyofanyika katika viwanja vya Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam Julai 7, 2023. Kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Temeke, Kidawa Masoud na wa pili kulia ni Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Matawi ya Benki ya NMB, Donatus Richard.
Na Mwandishi Wetu
Jumla ya washindi 22 wa Kampeni ya uhamasishaji wa kuweka akiba ya Benki ya NMB 'Bonge la Mpango' wamekabidhiwa zawadi zao jijini Dar es Salaam.
Zawadi zilizokabidhiwa leo ni pamoja na bajaji za mizigo tano zenye thamani ya shilingi millioni 25, pikipiki 11 zenye thamani ya shilingi millioni 33, friji (jokofu) la kisasa la milango miwili, Smart Tv, mashine ya kufulia nguo, Laptop, simu ya Samsung Z Flip pamoja na simu ya iphone 14 ProMax.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo Mkuu wa Mtandao wa Matawi na Mauzo ya Rejareja wa Benki ya NMB, Donatus Richard alisema kampeni ya benki hiyo ilikuwa na lengo kuu la kuhamasisha uwekaji wa akiba na ililenga kukuza utamaduni wa kuweka akiba kwa wateja wake.
Richard alisema katika droo za awali za kampeni hiyo, benki yake ilitoa zawadi za shilingi milioni 110 kwa wateja wake 178 wakati wa kampeni hiyo iliyozinduliwa mnamo tarehe 29 Machi, 2023.
“Ili kurudisha faida tunayoipata kama benki kwa wateja wetu, tulizindua promosheni hii Tarehe 29 Machi na tumeshuhudia zawadi za pesa taslimu, vifaa mbalimbali vya kielektroniki zikiwemo friji, TV, pikipiki huku zawadi za pesa zikiwekwa katika akaunti za washindi, lengo likiwa kuhamasisha wateja kuendelea kuwa na akiba katika akaunti zao,” alisema Richard.
Kampeni hiyo ya uhamasishaji wa kuweka akiba ya Benki ya NMB iliyopewa jina la ‘Bonge la Mpango’ Msimu wa Tatu ilifikia kilele Julai 5, 2023 na kuwafanya wateja wenye bahati kushinda zawadi nono zenye thamani ya shilingi milioni 69.5 wakati wa droo kubwa ya kampeni hiyo iliyofanyika kwenye banda la benki hiyo katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment