HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 20, 2023

SERIKALI YAJIDHATITI KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAWEKEZAJI WA MADINI

Na Magrethy Katengu


Wizara ya Madini imesema itahakikisha inaweka mipango thabiti kutatua  baadhi ya  changamoto zilizopo kwenye Sekta ya Madini ikiwemo miundombinu  zinatatuliwa kwa wakati ili kusaidia Wawekezaji wanaongeza tija  uzalishaji wa madini nchini na Pato la Taifa kukua .



Ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko wakati akifungua kikao Wadau wa madini  cha kujadili maendeleo, changamoto na kero na inazozikabili Kampuni kubwa za kati zinazojishughulisha na uchimbaji wa madini nchini katiaka migodi mbalimbali hapa nchini. 


"Tumetumia siku pekee ya leo ya kuwasikiliza wachimbaji wakubwa wa madini na wa kati kama tunavyo wasikiza Wachimbaji Wadogo kama wanachangamoto gani ili tuweze kuzipatia ufumbuzi na pia tunajiandaa na Mkutano wa Mkuu wa Kisekta wa Mwaka unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu," amesema Dkt. Biteko.


Waziri  Biteko amesema tayari serikali imerahisisha mazingira ya kikodi kwa wachimbaji wa madini ili kuondoa utititi wa Kodi na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika kutimiza majukumu yao.


Kwa upande wake, Waziri wa Madini Maji, Nishati na Madini kutoka Zanzibar Staibu Hassan ameipongeza Wizara ya Madini kwa hatua kubwa wizara hiyo imekuwa mwalimu wa mataifa mengi kujifunza usimamizi bora wa shughuli za biashara na uchimbaji madini.


Naye, Mwenyekiti wa Chemba ya Migodi, Mhandisi Philibart Rweyemamu amesema Chama anachokiongoza kipo tayari kushirikiana na serikali ili kuondoa changamoto na kutoa na kupata suluhisho la kudumu  hatimaye kufikia lengo la kuchangia asilimia 10 kwenye Pato la Taifa ifikapo 2025 kama ilivyo azma ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan


"Kikao cha namna hii kitakuwa kinafanyika kila robo mwaka ili kutoa taarifa kwa serikali juu ya maendeleo ya shughuli zetu, kuueleza umma nini kinachofanyika pamoja na kuishauri serikali kitu gani tunafikiri kifanyike ili kurahisisha utendaji wa Sekta ya Madini," amesema Mhandisi Rweyemamu.


Katika kikao hicho Kampuni tano za uchimbaji mkubwa wa madini zimetoa taarifa za utekelezaji wa miradi inayotekelezwa ikiwemo Kampuni ya Nyati Corporation, Sotta Mining, Tembo Nickel Corporation, Twiga Minerals na Faru Graphite Limited.

No comments:

Post a Comment

Pages