HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 06, 2023

Tigo waanza kukopesha simu janja za Samsung

Na Tatu Mohamed, Dar es Salaam


MENEJA wa Vifaa vya Intaneti kutoka Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo, Imelda Edward, amesema wameamua kuanza kuwakopesha watanzania simu janja aina ya Samsung baada ya kubaini kwamba gharama imekuwa kikwazo cha watanzania wengi kumiliki kifaa hicho cha mawasiliano.



Akizungumza katika banda la Tigo, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa maarufu sabasaba yanayofanyika kitaifa mkoani Dar es Salaam, alisema kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Samsung wanawapa wateja wao fursa ya kulipia kiasi kidogo cha fedha na kumpatia simu, na kwamba kiasi kilichobaki ataweza kulipia kidogodogo kwa mwaka mzima.


“Pia mteja atapata ofa ya kifurushi cha intanente MB71 bure kwa mwaka mzima, hivyo tunatoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam na watanzania kwa ujumla kutembelea banda letu ili kujionea bidhaa mbalimbali,” amesema Imelda.


Msimamizi wa mauzo kutoka Samsung Tanzania Edwin Biampanjo, amesema simu hizo ni bora na zinasifa kubwa ya kutunza chaji muda mrefu na kwamba wanatoa warantii wa miezi 24.


“Mteja akikuta kunatatizo lolote ndani ya miezi 24 anaweza kupeleka kwenye kituo chetu cha huduma chochote simu yake itarekebishwa kwa muda mfupi na kama tatizo litakuwa kubwa zaidi atabadilishiwa na kupewa nyingine mpya bila gharama yoyote,” amesema Edwin.

No comments:

Post a Comment

Pages