HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 15, 2023

UDAHILI VYUO VIKUU 2023/2024 WAFUNGULIWA RASMI

Na John Marwa


Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kufunguliwa kwa dirisha la udahili kwa mwaka wa masomo 2023/2024 katika Shahada ya kwanza.

Akitangaza kufunguliwa kwa dirisha hilo leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa amesema dirisha la udahili kwa mwaka wa masomo ya Elimu ya Juu limefunguliwa leo Julai 15 hadi Agosti 4 2023.


"Kwanza kama nilivyosema tunapenda kuutangazia umma wa watanzania na wadau wengine wa Elimu ya Juu, ndani na nje ya nchi kwamba dirisha la udahili kwa shahada ya kwanza kwa mwaka 2023/2024 limefunguliwa rasmi kuanzia leo tarehe 15 Julai, 2023 na dirisha hili litakuwa wazi mpaka tarehe 4 Agosti, 2023. 


"Hii ni awamu ya kwanza ya waombaji wa udahili kwa dirisha la udahili kwa mwaka 2023/2024. Kwaiyo ni vizuri kuzingatia kuwa dirisha hili la kwanza litakuwa wazi kuanzia leo Julai 15 hadi Agosti 4, 2023." Amesema Prof. Kihampa na kuongeza kuwa.


"Katika hili tuzingatie utaratibu wa maombi ya udahili kwa mwaka wa masomo wa 2023/2024. Waombaji  wanaotarajiwa wako katika maeneo makubwa matatu, kwa maana ya sifa za wale ambao tunatarajia watatuma maombi ya kujiunga na Shahada ya kwanza.


"Kwanza kabisa ni wale wenye sifa stahiki za kidato cha sita, lakini kuna wale wenye sifa stahiki za Stashahada au sifa nyingine linganifu.


"Kundi la tatu ni wale wenye sifa stahiki za cheti cha awali kinachotolewa na Chuo Kikuu huria cha Tanzania, wenye sifa stahiki za cheti cha awali 'Foundation Certificate' katika utaratibu huo kuna maeneo makubwa mengine mawili.


"Kwamba maombi yanatakiwa kutumwa moja kwa moja kwenye Vyuo husika, na maelekezo mahususi yanapatikana katika tovuti ya Vyuo vilivyo ruhusiwa kudahili wanafunzi kwa shahada ya kwanza kwa mwaka 2023/2024." Prof. Kihampa amesisitiza kuwa.


"Nisisitize kwamba kama ilivyokuwa kwa miaka mitano mfululizo, waombaji wa udahili wa Shahada ya kwanza wanatuma maombi yao moja kwa moja kwenye Vyuo husika ambavyo vimeruhusiwa kudahili wanafunzi wa Shahada ya kwanza kwa mwaka 2023/2024.


"Waombaji wanaotaka kujua vigezo wanaweza kuingia pia katika tovuti ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ambapo watakwenda moja kwa moja kwenye vitabu vya miongozo ya udahili kwa mwaka wa masomo 2023/2024 vinajulikana kwa kiingereza kama 'Undergraduate Admission Guide Books' na pale hivi vitabu viko vya aina mbili. Kitabu cha kwanza ni kwa wale wenye sifa stahiki za kidato cha sita na kitabu cha pili kinaonyesha zile sifa zingine kwa maana ya Stashahada na wale ambao wana cheti cha Chuo Kikuu huria cha Tanzania." Amesema Prof. Kihampa huku akiwataka waombaji kuzingatia.


"Maswala muhimu ambayo waombaji wa udahili wanatakiwa kuzingatia, la kwanza kabisa ni kusoma miongozo na miongozo niliyoitaja hapa. Lakini miongozo mahususi inapatikana katika tovuti za Vyuo ambavyo vina sifa ya kudahili wanafunzi kwa mwaka wa masomo wa 2023/2024.


"Jambo lingine la tatu ni kwa waombaji wanapokutana na changamoto za uoambaji katika mifumo hiyo husika wawasiliane moja kwa moja na Vyuo husika. Vyuo hivi kwa miaka yote mitano mfululizo na mwaka huu pia wana madawati maalumu ya kuweza kuwasaidia waombaji kila wanapokutana na changamoto. Nitoe pia msisitizo kwa Vyuo kuendelea kuhakikisha kuwa madawati haya yanakuwa wazi ili pale waombaji watakapokuwa wanahitaji msaada wa aina yoyote waweze kusaidiwa." Hata hivyo amebainisha kuwa.


"Jambo lingine la kuzingatiwa ni wale waombaji wenye sifa zilizotolewa na Taasisi zingine za nje ya nchi kwa maana ya kidato cha sita, wawasilishe vile vyeti vyao Baraza la Mitihani la Tanzania ili kuweza kupata sifa linganifu. Lakini kuna wale wenye Stashahada ambazo zimetolewa na Taasisi zingine za nje ya nchi wanatakiwa wawasilishe  vyeti vyao Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi yaani 'NACTE' ili vyeti vyao viweze kufanyiwa tathimini ya kupewa ulinganifu kabla hawajatuma maombi yao katika Taasisi za Elimu ya Juu.


"Mwisho kabisa nitoe tahadhali, na tahadhali ni muhimu kuzingatia. Vyuo vya Elimu ya Juu nchini Tanzania vinapokea maombi ya wale wanaomba kudahiliwa katika Shahada ya kwanza moja kwa moja kupitia mifumo ya kielekitroniki ya tovuti zao. Hapa nina maanisha kwamba hakuna watu wa katikati ama maarufu kama madalali. Kwaiyo waombaji waaaswa kwamba waepuke wasije wakatapeliwa na watu   ambao ni madalali au mawakala. 


"Mwombaji anashauriwa aende moja kwa moja katika tovuti ya Chuo husika ataona jinsi ya kuweza kufungua akaunti yake na ataweza kuona sifa linganifu na vigezo vingine vyote vya kuzingatiwa kama vilivyotolewa na Chuo husika cha Elimu ya Juu." Amesema Prof. Kihampa 

No comments:

Post a Comment

Pages