HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 26, 2023

UNIVERSITIES ABROAD WATOA MCHONGO KWA TAIFA

Naibu waziri wa Elimu, sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga (kushoto), akimkabidhi cheti Mkurugenzi Mkuu Taasisi Universities Abroad Representative (UAR), Tony Kabetha, wakati wa kufunga maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia, yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Wawkilishi wa Vyuo vya Nje wakiwa katoka picha ya kumbukumbu na mgeni rasmi.

 

Na John Marwa

Watanzania wameshauriwa kuchangua masomo yenye soko na sio tu kuchangua ilimradi wamechangua katika masomo ya Elimu ya Juu ili kuweza kutimiza ndoto zao.


Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu Taasisi 'Universities Abroad Representative' (UAR), Tony Kabetha, katika kufunga maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia, yaliyofanyika wiki jana katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

"Kikubwa ambacho tumekiona hapa sisi na changamoto za vijana, ni kwamba wazazi tumewaamini hawa vijana wamemaliza masomo na tunawauliza ndoto yao ni nini, lakini ukiwauliza wao hawajui sawasawa nini wakasome Ili waweze kutimiza zile ndoto zao.

"Kwaiyo wenzetu wa TCU wametoa utaratibu mzuri wa kuweza kuwaelimisha lakini yawezekana vitabu ni vikubwa sisi tumezoea hayo ni rahisi kuchambua na kuwaelewesha kwaiyo ni kweli kuna changamoto kubwa sana kwa wazazi, msichangue tu ilimradi kuchagua, wachague kitu ambacho kina soko, teknolojia imebadilika kuna vitu leo vina soko kesho havina soko."

"Sisi tumekuwa tunashiriki kwa muda mrefu, maonesho ya mwaka huu yamekuwa mazuri kwa sababu matokeo yametoka na ufunguzi umeanza kwaiyo ni wiki njema kwa wanafunzi, wito ni kwamba tumekuwa na Vyuo vingi safari hii vya kutoka nje ambavyo tunaviwakilisha kwa maana ya taasisi mbalimbali." Amesema Kabetha na kubainisha kuwa

"Kipekee Universities Abroad tuna Vyuo zaidi ya 200 na tumesaini mkataba na bodi za Elimu barani Ulaya na India ama bara la Asia, kwaiyo kwa mara ya kwanza sisi tumekuwa na mikopo Sasa hivi, wanafunzi wataenda huko kusoma Poland pamoja na India kwa mkopo, mzazi anachangia kitu kidogo na sisi tunamdhamini anaenda na kuendelea kulipa kidogo kidogo huko shuleni.

"La pili kumeanzishwa taaluma maalumu hapa hazitolewi lakini zinahitajika sana hasa kwa wenzetu wa utabibu 'medical' kwamba kila aliyemaliza Sayansi anataka kuwa daktari lakini sasa hivi kuna u daktari unahitaji 'medical imagine technology' ambao ni wataalamu wa mambo ya kansa na wale wa kusoma vipimo ambavyo siku zote Tanzania au nchi zinazoendelea ukipimwa unaambiwa majibu ni baada ya wiki mbili au wiki tatu.

"Sasa hao wataalamu wanahitaji vijana waliosoma Sayansi au PCB, wataenda kusoma ama kwa ufadhili ama kwa mkopo nje." Kabetha ameongeza kuwa.

"Nitoe tu wito kwamba pamoja na taasisi nyingi zinazofanya kazi vizuri lakini Universities Abroad sisi tuko Mlimani City Jengo la Mlimani Tower, tunawakaribisha watanzania katika nafasi hizo rahisi na bora.

"Lakini niipongeze Serikali kwa sababu ya uwekezaji wao mkubwa kwa vijana wamefaulu vizuri mwaka huu kwaiyo kinachoangaliwa na wazazi kama ufaulu mkubwa basi tuangalie Vyuo kwa sababu ni nafasi unaweza ukaikosa lakini yale utakayo kosa hapa nje tunaweza tukakupeleka au kozi ambayo hapa haitolewi na ina soko sisi tanakupeleka nje.

"Kingine niseme kwamba vijana wetu wengi hawajajua ni nini cha kusoma Ili kupata ajira, vijana wengi wako mitaani na wmmefaulu vizuri wazazi wamewekeza ni kwa sababu moja kubwa, hawakujua soko la ajira linahitaji nini, tunatoa ushauri bure kwa Watanzania wote kupitia mitandao mbalimbali ukiweka tu Universities Abroad utapata tutakushauri wewe kama mtanzania na sisi kama wawekezaji kwa pamoja tuijenga Tanzania." Amesema Kabetha.

No comments:

Post a Comment

Pages