HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 15, 2023

USIPIME, JEZI ZA SIMBA SC KUZINDULIWA MLIMA KILIMANJARO

 Na John Marwa


Ni hatareee, ndivyo unaweza kuelezea mara baada ya Klabu ya Simba kutangaza mchana wa leo kuwa uzinduzi wa jezi yao ya msimu ujao watautambulisha juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro.


Hayo yamesemwa leo na Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Imani Kajula, amesema wanaenda kuzindua jezi kwa njia tofauti ambayo haijawahi kutokea.


"Tutaenda kuzindua jezi zetu katika njia tofauti. Sisi tunafanya vitu tofauti, haijawahi kutokea.


"Nawaambia rasmi hapa kwamba jezi ya Simba itazinduliwa juu ya Mlima Kilimanjaro. Itaanza kupandishwa siku ya jumatano na watakuwa kileleni siku ya ijumaa na juma mosi jezi itakuwa kwenye maduka yote nchini.


"Ijumaa saa 1:00 usiku jezi itakuwa imefika kileleni kwenye Mlima Kilimanjaro. Itazinduliwa na kuonekana siku hiyo"amesema Kajula.


Kwa kufanya hivyo Simba itakuwa klabu ya kwanza kufanya hivyo na itabaki kuwa historia nzuri kwa klabu hiyo ambayo ni klabu bora Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ikishika nafasi ya Saba Barani Afrika.

No comments:

Post a Comment

Pages