HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 15, 2023

SIMBA DAY YARUDISHWA NYUMA


Na John Marwa


Uongozi wa Klabu ya Simba umetangaza kuwa Simba Day mwaka huu itafanyika Agosti 6 badala ya Agosti 8 kutokana na ratiba ya Ngao ya Jamii.

Taarifa hiyo imetolewa na Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally mchana wa leo ambapo amesema wameridisha nyuma siku mbili sababu Agosti 10 watakuwa na mchezo wa Ngao ya Jamii.


"Simba Day itakuwa Agosti 6, tumerudisha nyuma siku mbili sababu Agosti 10 tutakuwa na mchezo wa Ngao ya Jamii, hivyo tunataka wachezaji wetu wapate muda wa kupumzika" amesema Ahmed.


Simba Day ilianzishwa mwaka 2009 ambapo imekuwa ikifanyika kila Agosti 8, kwa ajili ya kuwakutanisha wanasimba, kuwatambulisha wachezaji wa timu zao zote na mabenchi ya Ufundi huku ukipigwa mchezo wa kimataifa na klabu mwalikwa na kusindikizwa na Burudani kutoka kwa wasanii.

No comments:

Post a Comment

Pages