HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 06, 2023

WANACCM WATAKIWA KUJITOKEZA KUMLAKI MWENYEKITI UWT TAIFA MARY CHATANDA SONGEA MJINI JULAI 7


NA STEPHANO MANGO, SONGEA

 

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Pius Chatanda anatarajia kufanya ziara ya kikazi Julai 7 mwaka huu katika kata za Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mjini ili kujiuonea uhai wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na kukagua miradi ya maendeleo.

 

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana Ofisini kwake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Mjini Mkoani Ruvuma James Mgego alisema kuwa Mwenyekiti wa Uwt Taifa Chatanda akiwa ameambatana na Wajumbe wa kamati ya Utekelezaji wa Uwt Taifa watafanya ziara ya siku moja wilayani humo.


Mgego alisema kuwa katika ziara hiyo Mwenyekiti Chatanda atakagua miradi inayotekelezwa na Chama  pamoja na miradi inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya elimu, uchumi na miundombinu.

 

Alisema kuwa akiwa Wilayani humo Mwenyekiti Chatanda atapata fursa ya kufanya vikao vya ndani na viongozi wa mashina, matawi na kata, pamoja na kufanya mikutano ya hadhara na wananchi wa wilaya hiyo katika viwanja vya lizaboni.

 

Mgego aliwataka viongozi na wananchi wote kujitokeza kwa wingi kumlaki mgeni huyo na kuhudhuria kwenye mikutano ya hadhara itakayohutubiwa na Mwenyekiti huyo na viongozi wa ngazi ya juu ya Jumuiya hiyo ya UWT Taifa.

 

Alisema kwa namna ya pekee kabisa Ccm Wilaya ya Songea Mjini inampongeza Rais Dkt Samia kwa namna anavyopambana kuhakikisha huduma za kiuchumi na kijamii zinawafikia wananchi, pamoja na ujenzi wa miundombinu ya elimu, usafirishaji.

 

Naye Mwenyekiti wa Uwt Wilaya ya Songea Mjini Veneranda Nkwera alisema kuwa maandalizi ya kumpokea Mwenyekiti Chatanda kwenye kata zote ambazo amepangiwa kwenda yamekamilika na kwamba wanawake na wajasiriamali mbalimbali wanatakiwa kujitokeza kwa wingi ili kuja kusikiliza ujumbe aliokuja nao.

 

Nkwera alisema kuwa Vikundi mbalimbali vya wajasiliamali vitakuwepo pamoja na burudani kutoka pande mbalimbali za Songea Mjini vitakuwepo kwenye shamra shamra za mapokezi hayo

No comments:

Post a Comment

Pages