HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 25, 2023

CCM YAENDELEA KUTEKELEZA AHADI YAKE VINGUNGUTI

Na Magrethy Katengu

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Vingunguti Mhe Omary Kumbilamoto amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kitahakikisha kutekelezea Wananchi wake yale mazingira mazuri ukiwemo kujenga barabara za mtaa kiwango cha lami ,ujenzi soko la kisasa mtaa wa majengo na fremu 36 za mama lishe.



Ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa hadhara  na wananchi wa kata hiyo ambapo amesema Wakati wa uchaguzi wa 2020 Chama.cha Mapinduzi CCM kiliahidi kutekeleza mambo mbalimbali na walitekeleza kwani fedha zilitolewa milioni 200 za ujenzi wa mabucha ya kuuzia nyama ya ng'ombe pia bilioni 50 likaketwa gereneta pale machinjioni kusaidia umeme ukikatika .

Hata hivyo ameendelea kubainisha kuwa Serikali ya awamu ya 6 chini ya Dk. Samia Suluhu Hassan ilitoa billion 5 na miliion 800 kwa ajili ya kujenga barabara za kata hiyo kwa kiwango cha lami na kuletwa kwa maji safi hivyo Wananchi wasitishwe na maneno ya wapinzani waangalie kwa macho yale yanayotendwa na serikali yak waliyoiamini na kuipa dhamana kupitia chama cha mapinduzi CCM .

Katika hatua nyingine Omary Kumbilamoto ametoa bati 15 kwa ajili ya ofisi ya kata eneo la stoo pia laptop yenye thamani ya milioni moja na laki sita friji, sukari na majani ya chai hii ni kurahisisha watumishi wafanye kazi kwa weledi zaidi na kwa haraka

"Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM chini ya Mwenyekiti wake Rais Dkt Samia Suluhu Hassani katika kipindi kifupi miaka hii miwili tunajionea wenyewe miradi mikubwa ya kimaendeleo ikitekelezwa maisha malalamiko yaliyokuwa yasikiwa eti vyuma vimekaza yamekwisha kwani Mama Rais amekuwa akitafuta wawekezaji huku na kule kuleta unafuu wa maisha" amesema Mstahiki Meya Kumbilamoto

Aidha Mstahiki Meya ametoa wito kwa wananchi uchaguzi unakaribia wasitingishwe na maneno manenomaneno ya wapinzani kuwa miaka mitano mingine ya Dkt Samia Suluhu Hassani wampe Imani kutakakuwa na mabadiliko makubwa ya maendeleo zaidi ya hapo

Naye Miongoni mwa Mwanachi Danieli Damsoni ameshukuru sana kwa juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Chama cha Mapinduzi CCM licha ya yeye kuwa chama cha ACT wazalendo. lakini ukweli Imani yeke ni kubwa. kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassani ni kubwa hivyo aendelee kufanya kazi kwa. bidii maneno yataongewa vibaya lakini anamshauri Mti wenye matunda ndiyo hupigwa mawe .

"Kiukweli wanasiasa hasa upinzani hawatabiriki kipindi cha hayati Dk. John Magufuli walisema hafai kwa kuwa mikutano ya kisiasa ya hadhara ilifungiwa lakini sasa huyo aliyewaita na kukaa naye meza moja wengine walikimbia nchi akawarudisha warudi nchini  waendelee kufanya mikutano ya hadhara pasipo kutukana wala kudhihaki hao hao wamemgeukia na kuzunguka nchi nzima kumsema vibaya lakini amewacha waendelee hii ameonyesha ukomavu wa kisiasa" amesema Daniel mwanachama wa ACT wazalendo

Hata hivyo Wananchi wameshauriwa kufanya shughuli zao za kiuchumi kwa amani na utulivu kama Kuna kero zozote wasisite kusema Kwa viongozi wao wa ngazi za chini na zitafikishwa mahali husika na kutatuliwa kwa wakati kama ilivyokuwa mgogoro wa wafanyabiashara Kariakoo.


No comments:

Post a Comment

Pages