Na John Marwa
Klabu ya KMKM ya Zanzibar imeanza vibaya kampeni za Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL hatua za awali kwa kukubali kipigo cha mabao (1-2) dhidi ya St George ya Ethiopia.
Mtanange huo umelindima Dimba la Azam Complex, ambapo KMKM wameutumia kama uwanja wao wa nyumbani.
Mabao ya mchezo huo kwa upande wa wageni St George walianza kuzisalimia nyavu za KMKM dakika ya 39 kupitia kwa nyota wao Binyam Damte huku
Natnael Zaleke 53 dakika ya 53 akipiga chuma cha pili baada ya mabeki wa KMKM kushindwa kundosha mpira wa krosi.
KMKM hawakuwa wanyonge kipindi cha pili kwani walihanikiza mashambulizi mtawalia AA kufanikiwa kupata bao la kufutia machozi kwa mkwaju wa penati uliowekwa kimiani na Salum Salum dakika ya 75, baada ya mlinzi wa St George kuunawa mpira ndani ya boksi.
Kwa matokeo hayo KMKM wana kazi ya kufanya ili kuweza kusonga hatua ya mtoano kutinga hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL wiki moja ijayo nchini Ethiopia.
No comments:
Post a Comment