Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
MAWAKILI
Wazalendo wameunga mkono makubaliano baina ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu uendelezaji na
uboreshaji wa bandari Tanzania.
Akizungumza na wanahabari jijijini humo, Mwenyekiti wa Mawakili Wazalendo Juma Nassoro amesema katika makubaliano hayo serikali imefanya jukumu lake kwa kutekeleza mamlaka iliyopewa kwa mujibu wa katiba, sheria na desturi zinazotawala.
“Baada ya kufanya majadiliano, makubaliano yaliandaliwa na kusainiwa. Ibara ya 31 ya Makubaliano inahitaji makubaliano hayo kuridhiwa. Na hapa kwetu wenye mamlaka ya kuridhia ni Bunge chini ya Ibara ya 63 (3) (c) ya Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Wakili Nassoro na kuongeza,
“Bunge ndicho chombo ambacho kina wawakilishi wa wananchi. Na Bunge limeridhia makubaliano hayo baada ya kujadili kwenye vikao vyake na kuridhika kuwa makubaliano hayo yana manufaa makubwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”.
Amebainisha kuwa Serikali imetimiza wajibu wake na itaendelea kusimamia utekelezaji wake kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi.
“Nasi tunaunga mkono juhudi hizo za Serikali za kutafuta wawekezaji kutekeleza sera na sheria za nchi, tunaunga mkono na kupongeza hatua ya Serikali kutafuta ridhaa ya Bunge na kuruhusu mjadala wa wazi na maoni ya wananchi,” amesema na kueleza,
“Tunatambua utekelezaji wa makubaliano haya hayajaanza, kuna hatua kadhaa za kitaalam na kiufundi zitafuata. Watanzania hatuna sababu ya kutilia shaka utekelezaji wa makubaliano hayo,”.
Ameisistiza kuwa vipengele vinavyoleta mjadala, vimetafsiriwa vibaya aidha kwa makusudi yaliyojificha au bila kujua.
Ameeleza baadhi ya vifungu hivyo kuwa ni kuhusu ukomo wa muda wa makubaliano, bandari zitakazohusika, uhalali wa serikali ya Dubai kuingia makubaliano, umiliki wa ardhi, mtazamo wa sheria kuhusu makubaliano kuridhiwa na Bunge, mtazamo wa sheria kuhusu Serikali kusaini makubaliano na baadaye na Bunge na Faida za kuingia makubaliano.
Katika hatua nyingine, Jopo la Mawakili hao 10 likiongozwa
na Mwanasheria Juma Nassoro, linatazamia kuiomba mahakama kuwaruhusu
kuendesha kesi binafsi au kumuamuru DPP kuwafungulia mashtaka watu
wanaotumia lugha za matusi na ubaguzi katika mijadala hukusu Makubaliano
Kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu uendeshwaji wa Bandari ya
Dar es Salaam.
Mwanasheria
wa Kujitegemea Salim Aboubakar, wakati amesema kuhusu maeneo mbalimbali
ya makubaliano baina ya nchi hizo mbili katika ushirikiano wa bandari,
ambapo wamesema uamuzi huo wataufanya kutokana na uzalendo na taifa lao.
Kwa upande wake, Mwanasheria
wa Kujitegemea Yahya Njama, amewataka watu wote kuacha kuingiza siasa
na ubaguzi wa aina yoyote katika suala hilo, na kuwataka kuwasilisha
hoja mbadala pindi wanadhani uwekezaji huo hauna manufaa kwa taifa.
No comments:
Post a Comment