Mwenyekiti wa Uvccm wilaya ya Iringa,Aizack Kikoti akizungumza Lengo la ziara ya kata kwa kata. (Picha zote na Denis Mlowe).
MJUMBE wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Iringa, Dk. Tumaini Msowoya akizungumza kwenye uzinduzi wa ziara ya Uvccm wilaya ya Iringa.
NA DENIS MLOWE, IRINGA
MJUMBE
wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Iringa, Dk. Tumaini Msowoya amewataka
vijana wa Uvccm wilaya ya Iringa Mjini kujibu hoja kwa hoja juu ya
mambo mbalimbali ambayo yamekuwa yakiibuliwa na wapinzani juu ya
serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu chini ya Chama Cha
Mapinduzi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa
ziara ya Mwenyekiti wa uvccm wilaya ya Iringa Mjini Aizaki Kikoti tukio
lilofanyika kwenye kata ya Mtwivila eneo la dodoma road A , Dk. Msowoya
alisema kuwa ifike wakati vijana wa Uvccm wajibu hoja kwenye mitandao
ambapo wapinzani wamekuwa wakitumia kwa kiasi kikubwa
Alisema
kuwa endapo vijana wakitumika vyema kwenye kujibu hoja kwa hoja kwa
Yale ambayo yanaendelea kwenye mitandao itakuwa dawa kwa wale
wanaopotosha juu ya utendaji kazi wa serikali ya Mama Samia Suluhu
Hassan.
"Tuna viongozi makini wa Uvccm wilaya
ya Iringa endapo utaona hoja kwenye mitandao usijibu ili mradi umejibu
kikubwa kama huelewi mfate kiongozi wako mshirikishe ili uwe na majibu
yaliyosahihi kuliko kukurupuka" Alisema
Dr.
Msowoya alisema kuwa ifike wakati vijana wajue kwamba kesho Yao hujengwa
na Leo iliyo makini na kuwataka kuwa vijana ambao wajenge Leo ili kesho
iwe Bora Kwa manufaa ya nchi na jamii kwa ujumla.
Kwa
Upande wake, Mwenyekiti wa Uvccm wilaya ya Iringa ,Aizack Kikoti
alisema kuwa ziara itakuwa ya kata kwa kata, mtaa kwa mtaa ikiwa na
lengo la kauli mbiu ya "Usimseme mama Samia ni rais mwenye maono" .
Alisema
kuwa katika ziara hiyo watakuwa wanamzungumzia mambo ya maendeleo
ambayo yamekuwa yakifanywa na Serikali kwani kumekuwa na mambo ambayo
hayako sawa kwa baadhi ya watu kupotosha jamii juu ya maendeleo
yanayoletwa na serikali.
Alisema
kuwa lengo lingine ni kujenga ushirikiano miongoni mwa vijana na jamii
kwa ujumla katika kufanya kazi na kuleta maendeleo ya mkoa wa Iringa na
nchi kwa ujumla.
"Sisi kama vijana wa Uvccm
tupo, hivyo hatuna budi kama vijana kuungana na vijana wengine kwenye
kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo na wanajambo la kuunga mkono
katika kazi zinazofanywa na Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan na ndio
watu wa kumzungumzia mazuri yote ." Alisema
Kikoti
aliongeza kuwa wako tayari kumlinda rais kumsemea na kukisemea chama
kwa wale wote ambao wamekuwa wapotoshaji na kuelezea utelezaji wa ilani
ya ccm katika kata zote 18 za mkoa wa Iringa.
Aidha
aliwataka vijana kuilinda nchi na viongozi wote kwani suala la vijana
kwa sasa wanatakiwa kuelewa bila wao ni sawa na bure hivyo tafsiri kwa
vitendo vile ambavyo vinafanywa na rais.
Alisema kwamba vijana wasisubiri mtu kutoka nje aseme kuhusu yanayofanyika na Serikali kama wanaitakia mema nchi
Naye
Katibu wa Uvccm wilaya ya Iringa, Hussein A.Kimu aliwataka viongozi
kuwatumia vijana kwenye shughuli zao na kuachana na kuwatumia wahuni
ambao wamekuwa wakipotosha juu ya serikali Yao.
Aidha
alitoa masikitiko makubwa kwa baadhi ya viongozi ambao wamekuwa
wakipuuza mwaliko wa Uvccm pindi wanapoalikwa kwenye shughuli za vijana
Hali ambayo imekuwa sugu kwa Sasa kwa baadhi ya viongozi wa ngazi za
juu.
Katika uzinduzi huo Msowoya
alifanikiwa kuchangia kiasi Cha 250,000 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi
wa nyumba ya katibu wa Uvccm wilaya ya Iringa ambao vitu mbalimbali
vilichangwa na wanachama na madiwani ambapo mnec Salim Abri aliahidi
kutoa bati za jengo Zima.
....mwisho....
1.
MJUMBE wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Iringa, Dk. Tumaini Msowoya
akizungumza kwenye uzinduzi wa ziara ya Uvccm wilaya ya Iringa
2. Mwenyekiti wa Uvccm wilaya ya Iringa,Aizack Kikoti akizungumza Lengo la ziara ya kata kwa kata.
(Picha zote na Denis Mlowe)
No comments:
Post a Comment