Mtumishi wa Mungu Mchungaji Dioniz Karwani akiwa katika ibada ya shukrani katika Kanisa Baptist Omurushaka.
Na Lydia Lugakila, Karagwe
Waumini wa Kanisa la Kibaptist Omurushaka Wilaya Karagwe mkoani Kagera wamehimizwa kuwa na moyo wa shukrani kwa kumtolea Mwenyezi Mungu shukrani na fungu la kumi katika shida na raha.
Hayo yamebainishwa na mtumishi wa Mungu Mchungaji Dionizi Karwani wa Kanisa la Kibaptist Omurushaka katika ibada ya shukrani ikiwa ni siku chache baada ya kupokea ubarikio wa kichungaji.
"Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa makubwa na mengi aliyonitendea, Lakini kuna baadhi ya waumini wanajisahau katika kutoa shukrani wanapotendewa mema. wanamkumbuka Mungu wakati wanapokuwa na shida, lakini wakati wa raha watu hujisahau kumtolea Mwenyezi Mungu kwa kila wanachokipata; alisema hayo mtumishi wa Mungu wakati akihubiri.
Alienda mbali zaidi na kuyazungumzia makundi mbali mbali yakiwemo ya Wakulima, Wafanyabiashara, na Viongozi kuwa hujisahau katika kumtolea Mungu wanapokuwa wamefanikiwa katika kazi za mikono yao.
"Ukiangalia na kusoma neno la Mungu katika injili ya Luka mtakatifu sura ya 17:11-19, tunaona mkoma mmoja ndiye alirudi kwa Yesu kutoa shukrani, Lakini wale kenda hawa kurudi kutoa shukrani. " alisema Mch. Karwani.
Pia Aliwahimiza waumini kuwa na utaratibu wa kutoa shukrani kila mwaka na fungu la kumi kutoka katika mazao yao au walichojaliwa kulingana na jinsi Mungu alivyowabariki huku akiwahimiza kutokata tamaa pale wanapojaribiwa badala yake wamlilie Mungu kwa kuomba na kutubu. Alisoma neno kutoka 1Samweli 7:8, na 12 "....hata Sasa Bwana ametusaidia."
Aidha aliwahimiza waumini hao kuendelea kuliombea taifa ili amani idumu pamoja na viongozi wake ili waendelee kuiongoza Nchi kwa amani na upendo.
Naye Mzee wa Kanisa la kibaptist Pius Bechumira aliwashukuru waumini hao kutokana na namna walivyopambana hadi kufanikisha tukio la ubarikio wa mtumishi wa Mungu Dioniz Karwani ambapo ibada hiyo imepambwa na kwaya mbali mbali ikiwemo kwaya ya upendo katika nyimbo zilizobeba ujumbe wa kuifanya kazi ya Mungu kwa moyo bila kusita na kutokata tamaa.
No comments:
Post a Comment