Temeke, Dar es Salaam, Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa Temeke imeshiriki Mashindano ya Polisi Jamii Cup
ambayo yamekuwa yakifanyika kuanzia tarehe 4 hadi tarehe 24 Septemba.
Mashindano hayo yamekuwa yakilenga kuimarisha mahusiano kati ya jeshi la
polisi na jamii. Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke imeweza kutoa vifaa
tiba na kufanikisha zoezi la uchangiaji damu kwa wanafunzi wa Chuo cha
Polisi(DPA) na wakazi wa eneo la Temeke waliojitokeza.
Mchango
muhimu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke katika mashindano haya
umegusa maisha ya watu na jamii nzima kwani Hospitali hii imefanikiwa
kukusanya jumla ya unit 290 za damu, jambo ambalo limechangia kwa kiasi
kikubwa kuongeza akiba ya damu inayohitajika katika huduma za matibabu.
Akizungumza
katika kuhitimisha mashindano hayo, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa Temeke, Dr. Joseph Kimaro, ameshukuru sana uongozi wa Chuo cha
Polisi Dar es Salaam (DPA) kwa kuleta pamoja wizara mbili muhimu, Wizara
ya Afya na Wizara ya Ulinzi, katika kuleta maendeleo ya taifa.
Amesisitiza kuwa michezo kama hii ina jukumu kubwa katika kujenga
mazingira rafiki kati ya jeshi la polisi na jamii.
Kwa upande
wake Mgeni Rasmi, SACP Mambosasa ambae pia ni Mkuu wa Chuo cha Polisi
Dar es salaam(DPA) amesema kuwa, kupitia michezo kama hii itasaidia
kuokoa vijana wetu katika wimbi la kujihusihsa na uhalifu hasa wa madawa
ya kulevya na vilevile kufungua fursa zitokanazo na michezo.
Aidha,
SACP Mambosasa amesema kuwa kupitia michezo hii wanaokoa maisha ya watu
wanao hudumiwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa Temeke, kwani
mashindano haya yameamabatana na uchangiaji damu wa hiari kwa lengo la
kujenga uwezo katika benki ya damu salama na kuendelea kuokoa wahanga wa
ajali, kina mama wanao jifungua na wagonjwa wengine
September 24, 2023
Home
Unlabelled
TEMEKE HOSPITALI YAKUSANYA UNIT 290 KATIKA MASHINDANO YA POLISI JAMII CUP
TEMEKE HOSPITALI YAKUSANYA UNIT 290 KATIKA MASHINDANO YA POLISI JAMII CUP
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment