Na Neema Adrian
Kuelekea maadhimisho ya miaka 78 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, shirika hilo limesemw kuwa litaendelea kuchagiza matumizi ya teknolojia za kisasa katika kutanua wigo wa ajira kwa vijana na hivyo kuchagiza maendeleo endelevu
Akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mratibu Mkazi wa UN Zlatan Millisic amesema shirika hilo limekuwa likishirikiana na taasisi pamoja na mashirika binafsi katika kuwawezesha vijana wabunifu kwenye sekta ya teknolojia ili kuwasaidia kupata ujuzi na kujiajiri ili kuboresha maisha yao"'Tumejipanga kuwaongezea uelewa vijana hawa ili kuwa na vigezo vinavyotakiwa katika kupata mikopo kutoka taasisi za kifedha na hivyo kuongeza ushiriki wao katika maendeleo endelevu," amesema.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sahara Ventures Mussa Kamata amesema wako tayari kuboresha sekta za Ubunifu, Uwekezaji pamoja na Ujasiriamali kwa vijana ikiwa ni pamoja na kubadilisha mawazo ya kibunifu ya vijana kuwa tija iliyokusudiwa kwa ustawi wao na taifa kwa ujumla.
"Tumekuwa tukishirikiana kwenye nyanja mbalimbali hasa katika kutimiza malengo 17, katika sekta ya ubunifu, ambapo vijana watatoa mawazo Yao yanafanyiwa maboresho mpaka kufikia hatua ya kuwa kampuni hii inaleta hamasa na vijana wanapata ujuzi na kwenda kujiajiri au kuajiriwa na pia tunawahamasisha vijana wa kike nao waje ili waweze kupata mawazo mbalimbali ya kiubunifu," amesema Bw.Kamata.
No comments:
Post a Comment