HABARI MSETO (HEADER)


October 23, 2023

Dulla mbabe 'amtamani' Katompa pambano Sisi kwa Sisi

Na Neema Adrian, Dar-es-Salaam


Pambano la 'Sisi kwa Sisi'  lenye lengo la kutangaza utalii kupitia mchezo wa ndondi bondia  Abdallah Pazi maarufu kama "Dulla mbabe linatarajiwa kufanyiaka Novemba 25, 2023 jijini Arusha.


Akizungumza na Waandishi wa habari mapema Leo Oktoba 23,2023  Promota wa pambano hilo kutoka Kampuni ya Lady in red Sophia Mwakagenda amesema lengo la Pambano hilo ni kutangaza Vivutio vya Utalii vilivyopo nchini Tanzania.


"Pambano hili madhubuti kwa ajili  ya kutangaza utalii wa ndani, ndiyo maana tumepeleka Arusha lakini kuendeleza vipaji vya vijana wetu kutokana na ukubwa wa  mabondia ambao wanacheza siku hiyo utalii wa nchini utazidi kufahamika nje ya mipaka ya Nchi yetu,"amesema mwakagenda.


Pia amesema  pamoja na Pambano hilo  kutakuwa na mapambano mawili ya wanawake kwa ajili ya kuonyesha uwezo wao katika masumbwi.


Hata hivyo bondia Dullah Mbabe amesema amejipanga vyema kuhakikisha analipiza kisasi kutoka kwa mpinzani wake, Katompa.


" Nilikuwa nataka pambano kati yangu Mimi na bondia  Katompa   kabla ya mwaka kuisha bondia ili tuweze kumaliza kisasi chetu hii sasa ndio fursa kwangu na mashabiki wangu kuona nalipa kisasi hiki Arusha na hii kuwa ni kwa mara ya kwanza nitaenda kutembelea vivutio vya utalii na fursa ya kipekee kama mzalendo na Mtanzania kutumia kipaji chake (Masumbwi) kutangaza Utalii kama alivyofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu kupitia Filamu ya "Royal tour ".


Mapambano mengine pia watapanda ulingoni ambao  ni Shaban Kaoneka,Lauren Japhet, Jacob maganga na wengine wengi.

No comments:

Post a Comment

Pages