Chama cha ACT Wazalendo kimeielekeza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho kuichambua Miswada ya Sheria kuhusu Uchaguzi, Tume ya Uchaguzi na Vyama vya Siasa iliyosomwa kwa mara ya kwanza Bungeni tarehe 10 Novemba 2023.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo kwenye Mkutano Mkuu wa Jimbo la Ilala uliofanyika leo tarehe 12 Novemba 2023 katika Ukumbi wa Simple Motel, Ilala, Dar es salaam.
"Ni jambo la faraja kuwa hatimaye miswada hii imewasilishwa Bungeni. Yapo masuala yaliyotufurahisha kama vile kuondosha suala la kupita bila kupingwa. Lakini, yapo masuala yanayohitaji maboresho ili kuhakikisha chaguzi zijazo zinakuwa huru, za haki na kuaminika. Chama chetu kitafanya uchambuzi wa kina wa miswada yote mitatu. Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Chama imeagizwa kufanya uchambuzi huo ambao utawasilishwa kwenye vikao vya Chama kabla ya kuwasilishwa Bungeni" alisema Ado Shaibu.
"Tunapenda pia kurudia rai yetu kuwa itakuwa ni jambo la ajabu kwamba Tume ya Uchaguzi itayoundwa isisimamie Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. ACT Wazalendo hatuungi mkono uchaguzi wa Serikali za Mitaa kusimamiwa na TAMISEMI" alisisitiza Ndugu Ado.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa ACT Wazalendo inaongozwa na Wakili Omar Said Shaaban ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar akisaidiwa na jopo la Mawakili wa Chama.
Mbali na hayo, Katibu Mkuu Ndugu Ado Shaibu amesema kuwa Chama cha ACT Wazalendo kinaendelea na chaguzi katika ngazi ya majimbo akiweka bayana kuwa Ilala inakuwa Jimbo la 80 kukamilisha Uchaguzi.
"Mwezi Machi 2024, ni mwaka wa kukamilisha uchaguzi wa Chama ngazi ya Taifa. Hadi kufikia mwisho wa mwezi Desemba 2023, majimbo yote 264 yatakuwa yamekamilisha chaguzi zake. Baada ya hapo tutafanya chaguzi za Mikoa na mwishowe chaguzi za Taifa Mwezi Machi mwishoni" alihitimisha Ndugu Ado.
Imetolewa na Janeth Joel Rithe, Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, ACT Wazalendo.
12 Novemba 2023.
November 12, 2023
Home
Unlabelled
ACT WAZALENDO KUICHAMBUA MISWADA YA UCHAGUZI
ACT WAZALENDO KUICHAMBUA MISWADA YA UCHAGUZI
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment