HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 13, 2023

FUKUTO LA JOTO MSIMBAZI LAMUIBUA AMBAGILE

Na John Marwa

Wakati Fukuto likiwe limetanda mitaa ya Msimbazi Mchambuzi wa Michezo nchini kutoka Wasafi FM George Ambagile amesema kufanya kazi Simba ama Yanga lazima kuwe na presha, hivyo ni wa kuwapima ukomavu viongozi wa Simba.


Kinachoendelea Unyamani ni baada ya kupokea kipondo kutoka kwa mtani wake Yanga SC cha mabao (1-5) mchezo ulipigwa Novemba 5 katika Dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

"Binafsi yangu sidhani kama inawezekana kufanya kazi Simba au Yanga bila presha ya mashabiki. Yani kama hutaki kupata presha kwa mashabiki basi kafanye kazi kwenye klabu tofauti na hizi klabu mbili."


"Na sio kwa Tanzania tu, kwa nchi yeyote ukienda kisha ukaambiwa hii ni klabu kubwa hapa nchini basi tegemea presha kubwa kutoka kwa mashabiki, yani ikishakuwa klabu kubwa basi ni klabu yenye mashabiki, mashabiki wenye mitazamo tofauti. Kama hautaki presha kubwa basi tafuta klabu ndogo, huko utafanya kazi miguu ikiwa juu."


"Na hiki ndicho kipindi hawa viongozi tunajua kwa kiasi gani wana utimamu wa akili, kuendana na presha ya mashabiki kipindi hiki ndicho kipindi cha kujua ubora na utimamu wa kiongozi.

Kiukweli sio kipindi rahisi na sitamani hata kuvivaa viatu vya viongozi wa Simba sababu ni kipindi kigumu mno." Amesema mchambuzi wa soka George Ambangile.


No comments:

Post a Comment

Pages