HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 09, 2023

Masheha Zanzibar watakiwa kushirikiana na Waratibu kupinga vitendo vya udhalilishaji

Masheha Zanzibar wametakiwa kushirikiana vyema na waratibu wa kupinga vitendo vya udhalilishaji ambao wanafanyakazi katika Shehia mbali mbali za Unguja  na Pemba ili changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa Majukumu yao ziweze kutatuliwa kwa wepesi/urahisi.


Akizungumza mmoja kati Maafisa  kutoka Divisheni ya Maendeleo ya Jamii ndugu Omar Haji Omar wakati walipofika kutambulisha kazi za Idara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto katika shehia, kwa Mashesha na Waratibu wa shehia kwa Wilaya ya kati Unguja, amesema mashirikiano yao yatawezesha kutatua changamoto kwa haraka.


Amefahamisha kwamba shughuli zote za  maendeleo au changamoto ya jamii katika shehia zao zinapaswa kuripotiwa katika Wizara husika lakini mashirikiano yao yatawezesha Wizara ya maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto kufanya kazi kwa ufanisi.


Amesema utaratibu huu umekuja baada ya kuundwa kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ikiwa miongoni mwa shughuli zake ni kutambua na kusimami shughuli zote za maendeleo ya jamii katika shehia zao zinatambuliwa na Wizara hiyo.


Amesmea ni lazima kuhakikisha kuwa shughuli zote zinazofanyika katika shehia zao wanaziwasilisha kupitia katika Wilaya ili nao waweze kuziwasilisha katika Wizara husika.


Amesema wanatambua kuwa masheha wanafanya kazi kubwa katika jamii, hivyo katika kuendeleza maendeleo mbalimbali katika shehia zao, ni lazima kuondoa changamoto baina ya masheha na waratibu ili  wafanye kazi zao vizuri kwa kwa kuleta ustawi mzuri kwa jamii.


Amesema lengo ni kuona maendeleo yote yanayotaka kufanyika na yaliyofanyika yanatambuliwa na kuona kila penye uhitaji wa huduma zinafikiwa kupitia shehia zao ili kupunguza matatizo madogo madogo yanayojitokeza.


Kwa upande wao Masheha wameonesha kufurahishwa kuwepo kwa utaratibu huo kwani awali haukuwepo na kusema kuwa wamepata usaidizi mzuri juu ya utendaji wao wa kazi.


Wamesema suala la kuripotiwa masuala ya Maendeleo ya Jamii katika shehia zao haufanyiki kwani hata wao baadhi ya shughuli hawashirikishwi, hivyo utaratibu huo utawasaidia wao katika kupata taarifa  sahihi za kumsaidia Rais katika kuelezea masuala mbalimbali ya Maendeleo yanayofanyika katika nchi kwa ujumla.


Nao waratibu wamewaomba Maafisa hao kuwafikishia utaratibu huo viongozi wao wa siasa wakiwemo Wabunge na Wawakilishi kuhusu miradi yao wanayoitoa katika shehia zao kuwashirikisha na Masheha pamoja na waratibu kwani wao ndio wahusika wakuu wa shehia.

No comments:

Post a Comment

Pages