HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 25, 2023

NMB Mlipa Kodi Mkubwa na Bora Zaidi Tanzania 2023 🇹🇿

 

Jana Tarehe 24 November  2023 kwenye siku ya Mlipa Kodi 2023, Benki ya NMB iliibuka Mshindi wa Jumla Kitaifa, kama Mlipa Kodi Mkubwa Zaidi Tanzania na kama Mlipa Kodi Bora Zaidi anayelipa Kodi kwa hiari (Most Compliant Tax Payer).

Huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa Benki ya NMB kupata tuzo hizi.

Jumla ya Tuzo ilizopata Benki ya NMB ni:

1️⃣ Mshindi wa Jumla Kitaifa: Taasisi inayolipa Kodi kubwa zaidi nchini Tanzania (Sekta zote).

2️⃣ Mshindi wa Jumla Kitaifa: Taasisi Bora inayolipa Kodi kwa hiari kwa  kuzingatia misingi na kanuni bora za ulipaji kodi (Most Compliant Tax Payer).

3️⃣ Mshindi wa Kwanza: Mlipa Kodi mkubwa zaidi katika kundi la Taasisi za Fedha nchini Tanzania (mara ya tatu mfululizo).

Akiongea mara baada ya kupokea tuzo hizo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna alisema tuzo hizo ni matokeo chanya ya misingi imara ya utawala bora na uadilifu, kuzingatia kanuni za ulipaji kodi, ufanisi katika kuendesha biashara na ubunifu wa suluhishi bora za kifedha kwa wateja.

Bi. Ruth Zaipuna alisema:  
“Nawashukuru wateja wetu na Watanzania wote kwa kuendelea  kuiamini Benki ya NMB kama mshirika wao kwenye biashara na shughuli zao, naishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya kufanya Biashara nchini na kipekee nawashukuru wafanyakazi wenzangu wote wa Benki ya NMB kwa kuendelea kufanya kazi kwa ari, bidii na kwa uzalendo mkubwa kwa maslahi mapana ya Benki na nchi yetu kwa ujumla.”

Tuzo hizo za Mamlaka ya Mapato Tanzania zimetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Dotto Biteko katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Kama mdau wa maendeleo, Benki ya NMB tutaendelea kuendesha biashara yetu kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi ili kuendelea kuchangia kikamilifu ujenzi wa uchumi wa Taifa letu.

#NMBKaribuYako



No comments:

Post a Comment

Pages