HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 14, 2023

Mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa (GDP) wafikia asilimia 9.1 mwaka 2020


Hongera Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuadhimisha miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Umoja na mshikamano ni chachu ya maendeleo ya Taifa letu. Leo, hapa Dodoma, tumeshiriki katika Mkutano wa Kwanza wa Kitaifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. 

 

Kupitia Mkutano huu, Mhe. Anthony Mavunde, Waziri wa Madini amechukua fursa ya kutafakari (reflect) utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. 

 

Wizara ya Madini imefanikiwa katika mambo kadhaa nayo ni: 

 

1. Mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa (GDP) umefikia asilimia 9.1 kwa mwaka 2022.

 

2. Ukuaji wa Sekta ya Madini umefikia asilimia 10.9% kwa mwaka 2022. 

 

3. Thamani ya madini yaliyouzwa nje ya nchi kwa mwaka 2022 yalifikia dola za Marekani bilioni 3.4 ambayo ni sawa na asilimia 56 ya mauzo yote ya bidhaa nje ya nchi. 

 

4. Ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali kwa mwaka 2022/23 yalikuwa bilioni 678. 5. Mapato ya kikodi yaliyopatikana kutokana shughuli za madini ni shilingi bilioni 808.9 mwaka 2022/23. 

 

Aidha, tunampongeza Mhe. Prof.Kitila Mkumbo kwa kuteua timu ya wataalamu ya uandaaji na uandishi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050. Timu hii imejaa wabobevu na watu mahiri. Tunawapongeza wateule wote. Vilevile, Wizara ya Madini itashirikiana kwa karibu na timu hii. 

 

Kupitia ushirikishwaji huo tuna imani kuwa Sekta ya Madini itakuwa ni kitovu cha maendeleo ya taifa letu na kutoa mchango mkubwa zaidi kwenye uchumi wetu. Madini ni Maisha na Utajiri. Katika miaka ya karibu tunakusudia yafuatayo: 

 

A. Tanzania kuwa kinara wa madini mkakati barani Afrika.

B. Tanzania kuwa kinara wa madini ya vito barani Afrika.

C. Sekta ya Madini kuzifungamanisha sekta nyingine zote katika uchumi wa taifa letu. Kadhalika, Wizara ya Madini itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi katika kuendeleza na kukuza uchumi wa Tanzania kupitia sekta ya madini.

No comments:

Post a Comment

Pages