Katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Fatma Hamad Rajab, akipokea Masaada wa Traki Suti kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Zanzibar, Naima Shaame ikiwa ni sehemu ya udhamini wa benki hiyo katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar pamoja na sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Hafla hiyo fupi ilifanyika ofisi ya wizara ya michezo Zanzibar.
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya NMB imetoa zaidi ya shilingi milioni 200 kwa ajili ya zawadi za mashindano ya kombe la mapinduzi Zanzibar na Traki suti 150 kwaajili ya kuvaa kwenye matembezi siku ya Mapinduzi.
Fedha
hizo kwa ajili ya bingwa ambaye atazoa shilingi milioni 100 mshindi wa
pili milioni 70, pamoja na medali za mabingwa na mshindi wa pili.
Akizungumza
wakati wa halfa ya kukabidhi nguo za mazoezi kwa ajili ya siku ya
mazoezi kitaifa yatakayofanyika Januari 1, ambazo zilimetolewa na benki
hiyo Meneja Biashara Zanzibar benki ya NMB Naima Said Shaame .
Alisema
udhamini huo unalenga azma ya benki ya NMB na pia juhudi za Serikali
katika kusherehekea miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema
benki ni miongoni wa wadau wakubwa inayochangia ukuaji wa wa sekta
mbalimbali za maendeleo Zanzibar, hivyo waliona ni wajibu wao kuwa
sehemu ya maadhimisho ambayo kilele chake ni Januari 12.
‘’Kama
Benki tunasema huu sio mwisho wa udhamini wetu. Tunaamini kwamba
michezo sio tu inachangia ustawi wetu, lakini pia inatuleta pamoja kama
taifa’’aliongeza.
Alisema
NMB imeamua kutoa Traki suti hizo za mazoezi 150 kwa jili ya kuunga
mkono siku ya mazoezi ikitaifa jambo ambalo hulifanya kila mwaka,
kuonyesha kuwa mazoezi ni muhimu kwa wananchi ambao ni wateja wao.
‘’Tunapenda
kuwa na wateja wenye afya na tunajua kuwa mazoezi ni afya, hivyo
tumeamua kuunga mkono jambo hilo ili kuhakikisha wateja wetu wanakuwa na
afya njema’’alisema.
Akizungumza
baada ya kupokea Traki suti hizo Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab, aliishukuru benki ya NMB kwa
misaada mbali mbali inayotoa.
Alisema
benki hiyo ni kiongozi wa kutoa misaada kwa serikali katika nyanja zote
za michezo na jamii, hivyo msaada huo umekuja wakati muafaka kwani siku
ya mzoezi ya kitafa ni siku kubwa.
Katibu
Fatma alisema amepokea misaada hiyo kwa furaha, ambapo ameitaka benki
hiyo kuendelea kusaidia kwani bado kuna mahitaji mengi yanatakiwa
kuendeleza michezo Zanzibar.
No comments:
Post a Comment