HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 20, 2023

WAARABU WAONANA NA ONANA BENJAMIN MKAPA.

 

Na John Marwa


Hatimaye wekundu wa Msimbazi Simba wamerejea kwenye gia ya ushindi kwenye michezo ya Kimataifa baada ya kuichapa Wydad Casablanca ya  Morocco  mabao 2-0.


Ni ushindi wa kibabe kwa Mnyama Simba kwenye Dimba la Benjamin Mkapa jioni ya leo kupitia Willy Essomba Onana ambaye ameweka kambani mabao yote mawili katika kipindi cha kwanza.


Kipindi cha pili Kocha Mkuu wa Simba Abdulhak Benchika aliamua kupaki basi na kuwasubiri Wydad kuwafungua jambo ambalo halijawezekana mpaka filimbi ya mwisho ya mchezo huo.



Kwa ushindi huo Simba wamefikisha pointi tano nyuma ya vinara Asec Mimosas ya Ivory Coast wenye pointi saba huku usiku huu wakiwa nyumbani kuwakabili Jwaneng Galaxy ya Botswana.


Kipigo hicho kwa Wydad kinawafanya kubuluza mkia wakiwa na alama tatu nyuma ya Jwaneng Galaxy nafasi ya tatu na alama zao nne.


Mnyama Simba atarejea dimbani mwakani kuwafuata Asec Mimosas kabla ya kuja kumalizana na  Jwaneng Galaxy Benjamin Mkapa ambapo mwezi wa pili 2024.


Ni ushindi wa kwanza kwa Kocha Bennchika tangu achukue mikoba ya kukinoa kikosi cha wekundu wa Msimbazi Simba katika michuano ya kimataifa huku ukiwa wa kwanza pia kwa Mnyama Simba msimu huu akiwa amecheza mechi nane sare sita, kipigo kimoja na ushindi moja.

No comments:

Post a Comment

Pages