HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 27, 2023

Wazazi waaswa kuwachunguza watoto wao

 


Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto bi Abeida Rashid Abdallah (Kushoto) akimkabidhi  cheti cha shukran Mratibu wa mafunzo ya kuwajengea uwezo kikundi cha Banaty Bi Raya Hamad Mchele, Mafunzo hayo yamefanyika Jana, katika ukumbi wa Michenzani Mall Unguja. 

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto bi Abeida Rashid Abdallah (Kati) akiwa katika picha ya pamoja na wanakikundi cha Banaty baada ya kuwakabidhi cheti cha Shukran katika mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika Jana, Michenzani Mall Unguja. 


Na Talib Ussi


Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto bi Abeida Rashid Abdallah amewataka Wazazi na Walezi Wanawake kuwachunguza watoto wao sehemu za siri katika miili yao ili kuhakikishwa kwamba wako salama na hawajafanyiwa vitendo vya udhalilishaji vya aina ya ngono.


Kauli hiyo ameitowa katika mafunzo ya kuwajengea uweza kikundi cha Banaty yaliyofanyika Michenzani Mall Unguja mara baada ya mtaalam wa Afya Dkt Ummulkulthum Omar kuwasilishaji mada ya afya ya mfumo wa uzazi pamoja na kueleza kwamba katika utekelezaji wa majukumu yake anakutana na kesi za watoto wachanga  wa miezi minane wameingiliwa kinyume na maumbile na kuharibiwa.


Bi Abeida amesema kwa vile Wazazi na Walezi Wanawake hawana vibakio ni vyema kuwa karibu na watoto hasa watoto wa kiume waliyofikia umri wa balegh kwa kuwauliza masuali bila ya kuona haya pamoja na kuwaangalia sehemu zao za siri kama ziko salama na hazijafanyiwa udhalilishaji wa aina ya ngono.


“Tuwe karibu nao hasa watoto wa kiume sisi wanawake hatuna vibakio kwahiyo lazima tuwe karibu na watoto wetu tuwahoji Je hakuna mtu aliyeguza sehemu za siri? Na tusiishie kuwauliza tu. Pia kuwaangalia hasa huko sehemu ya siri  tujue kama kuko salama, tusisuniria azoeshe mchezo mchafu ”. Alisema Abeida.


Alieleza kwamba ripoti ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeonesha matukio ya udhalilishaji 199 yameripotiwa kwa mwezi wa Oktoba, 2023 kati ya idadi hiyo asilimia 78.9 ni watoto na wanawake ni asimia 16.2 hivyo ni vyema Wazazi na Walezi Wanawake kila mara wawe karibu na watoto wao.


Aidha katibu Mkuu huyo alitoa wito kwa  washiriki wa mafunzo hayo  na wanawake wote waliyopata mafunzo ya ujasiriamali  kutumia ipasavyo  elimu hiyo kwani Serikali ya Mapinduzi inatoa fursa ya mikopo kwaajili ya kuwawezesha  kiuchumi  ili waweze kujiongezea kipato na kujikwamua na umasikinini. Alisema kwani umasikini pia unachangia matendo ya udhalilishaji kutokea kwa watoto.


Naye Mtaalum wa Afya bi Dkt Ummulkulthum Omar kutoka Hospital ya Rufaa ya Mnazimmoja Zanzibar katika mada ya mfumo wa uzazi aliyowasilisha alieleza matatizo  mbali mbali yanayowatokea wanawake katika mfumo wa uzazi ikiwemo kutoshika mimba, kutokwa na uchafu usiokuwa wa kawaida katika sehemu za siri, n.k. hivyo amewataka wanawake kukimbilia hospitali endapo wataona dalili yeyote ambayo sio ya kawaida kutokana na elimu aliyofundisha ili kuwahia kutimbiwa.


Aidha katika uwasilishaji wa mada hiyo aliezea kwamba anakutana na kesi ya watoto wa umri tofauti ambao wameingiliwa kinyume na maumbile ikiwemo watoto wa miezi minane, hali ambayo inasikitisha hasa ukiangalia matendo hayo yanafanywa na mtu wa karibu.


Mapema Mratibu wa mafunzo hayo ambaye ni Mkurugeni wa Raha online TV bi Raya Hamadi Mchele amesema lengo la kunadaa mafunzo hayo ni kuwapa elimu kundi la Banaty ikiwemo elimu ya afya, kujitambua na elimu ya ujasiriamali ili waweze kujikwamua kimaisha.


Kikundi cha Banaty kimeanzishwa kwa lengo la kusaidiana katika shughuli mbali mbali za kijamii ikiwemo harusi na msiba. Hivyo kikundi hicho kinamuda wa miaka minane na mfuko wao wafedha una pesa zaidi ya shilingi za Tanzania milioni ishirini.

No comments:

Post a Comment

Pages