Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph Kolombo (katikati), akipokea sehemu ya msaada wa mabati 120 yenye thamani ya zaidi ya Sh. Mill. 4 kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper kwa ajili ya Shule ya Msingi Kiasi, hafla hiyo ilifanyika katika Ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo. Kushoto ni Meneja wa NMB Tawi la Kibiti, Raphael Mbuya, Afisa Elimu Msingi, Zakayo Mlenduka (kulia), Katibu Tawala Wilaya ya Kibiti, Maria Katemana (wa pili kulia). (Na Mpiga Picha Wetu).Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph Kolombo (katikati), akipokea sehemu ya msaada wa mabati 120 yenye thamani ya zaidi ya Sh. Mill. 4 kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper kwa ajili ya Shule ya Msingi Kiasi, hafla hiyo ilifanyika katika Ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo. Kushoto ni Meneja wa NMB Tawi la Kibiti, Raphael Mbuya, Afisa Elimu Msingi, Zakayo Mlenduka (kulia), Katibu Tawala Wilaya ya Kibiti, Maria Katemana (wa pili kulia). (Na Mpiga Picha Wetu).
Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph Kolombo, akipeana mkono na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper, wakati wa hafla ya kukabidhi mabati yaliyotolewa na benki ya NMB kwa ajili ya Shule ya Msingi Kiasi.
Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph Kolombo (wa pili kulia), akizungumza wakati wa hafla ya kupokea msaada wa mabati 120 kutoka Benki ya NMB kwa ajili ya Shule ya Msingi Kiasi iliyopo Kibiti Mkoa wa Pwani Januari 29, 2024. Kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, Hemed Magaro (kulia) na Katibu Tawala Wilaya ya Kibiti, Maria Katemana (wa pili kushoto). (Na Mpiga Picha Wetu).
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper (kushoto), akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa mabati 120 kwa ajili ya Shule ya Msingi Kiasi iliyopo Kibiti Mkoa wa Pwani Januari 29, 2024. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph Kolombo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, Hemed Magaro (kulia) na Katibu Tawala Wilaya ya Kibiti, Maria Katemana (wa tatu kulia). (Na Mpiga Picha Wetu).
Na Mwandishi Wetu, Kibiti
Benki ya NMB jana ilikabidhi msaada wa mabati 120 yenye thamani ya shilingi milioni 4 kwa Shule ya Msingi Kiasi iliyopo wilayani Kibiti ikiwa ni mwendelezo wa mkakati kabambe wa benki hiyo wa kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu nchini.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika Kibiti, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper alisema benki yake imejizatiti kuendelea kusaidia maendeleo ya sekta ya elimu kwa kuwa inaamini elimu ndiyo chachu ya mafanikio.
“Sisi kama Benki ya NMB tunaamini kuwa kusaidia ukuaji wa sekta ya elimu ni kitu muhimu ndiyo maana kwa miaka mingi sasa, benki yetu imeipa sekta hii kipaumbele katika mkakati wetu wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSI). Leo tunakabidhi mabati 120 yatakayotumika kuezeka madarasa katika Shule ya Msingi Kiasi na tunaamini msaada wetu utasaidia sana katika kuweka mazingira mazuri kwa wanafunzi na walimu,” Prosper alisema.
Prosper wakati wa hafla hiyo alisisitiza dhamira ya benki hiyo ya kuendelea kuchangiza thamani ya pamoja kwa wadau wake wote wakiwemo wanahisa, Serikali na jamii ambako benki hiyo inafanya kazi.
"Kama benki, tumeendelea kujitolea kufanya kazi kwa karibu na washirika wote wa maendeleo ikiwa ni pamoja na Serikali ili kuimarisha maendeleo endelevu katika maeneo tunayofanyia kazi," alisisitiza.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph Kolombo, wakati wa hafla hiyo, aliipongeza benki hiyo kwa msaada huo huku akisisitiza kuwa msaada huo umekuja kwa wakati kwani wilaya hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa mabati.
“Kwa sasa tunakabiliwa na upungufu mkubwa wa mabati katika Wilaya ya Kibiti ili kuwezesha ujenzi wa nyumba za watumishi wa Serikali wakiwemo walimu na watumishi wa sekta afya. Zaidi ya watumishi wa sekta ya afya 534 katika wilaya hii kwa sasa hawana nyumba. Naushukuru sana uongozi wa Benki ya NMB kwa mchango huu na nakiri kuwa umekuja kwa wakati ambapo tunauhutaji,” alisema.
Kanali Kolombo wakati wa hafla hiyo aliahidi kuwa wilaya yake itatumia vyema mabati yaliyotolewa huku akiendelea kuishukuru benki hiyo kwa dhamira yake ya kuendelea kuunga mkono mipango mbalimbali ya maendeleo inayoongozwa na Serikali katika maeneo mbalimbali nchini.
“Nawahakikishia kuwa hakuna hata kipande kimoja cha bati kitakachopokea,” alisema.




No comments:
Post a Comment