HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

March 30, 2026

HUDUMA YA DHARURA HOSPITALI YA DK. OLE LENGINE YAIMARISHWA


Kikosi Kazi cha dharura katika Hospital ya Dk. Ole Lengine kikionesha kazi zake ndani ya gari la kusaidia wagonjwa wa dharura.


Mkurugenzi wa Hospital ya Dk. Ole Bi Bertha Emmanuel akipewa mkono wa pongezi na Mtendaji kutoka manispaa ya Ubungo DK. Felister Kimolo, hii ni katika kuunga mkono ushirikiano wa huduma za afya kati ya serikali na sekta binafsi.


NA ASHA BANI


HOSPITAL I  ya Dk. Ole Lengine Memorial imeongeza gari mpya na ya kisasa ya kisasa ya huduma ya dharura (Ambulance).


Mkurugenzi wa Hospital hiyo, Bertha Emanuel  alisema wanayofuraha kuongeza gari hilo kwani inasaidia katika kuongeza ufanisi na huduma ya dharura kwa wagonjwa.

"Tunafuraha kwani kuongeza gari hilo ya huduma ya dharura inasaidia kwa wagonjwa wa eneo hilo wa maeneo ya jirani,"alisema Bertha.


Mgeni rasmi katika hafla ya makabidhiao hayo ni Mchungaji Ezekiel  Ngao aliyeambatana na mwakilishi wa ofisi ya  DMO Dk. Felister Kimolu ambapo kwa nyakati tofauti walipongeza hatua ya uongozi wa hospital hiyo ambayo inawasaidia wananchi kupata huduma nzuri ya haraka zaidi.

No comments:

Post a Comment

Pages