CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka vijana kujitokeza wa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi huku kikiahidi kuwapa fursa kwa kuwapitisha kwa kuwa wanao uwezo wa kuongoza.
Kauli
hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Makamu Mwenyekiti wa CCM
Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana katika mkutano mkuu maalumu wa
ukaribisho wa wananchama wapya 1,167 wa Seneti ya Vyuo Vikuu wa DIT,
CBE, IFM na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kutoka tawi la Kibasila,
Kata ya Upanga Mashariki.
Kinana
alisema Chama kinawategemea vijana kwa kuwa wanayo chachu ya mawazo kwa
Chama, hivyo wasifikiri kuwa kuna sehemu nyingine mawazo yatatoka bali
watambue kuwa wao ni taifa la leo.
Alisema
Chama kinawategemea kwa ushauri, kujenga hoja na kukosoa, hivyo
watambue wao ni watu wa kisasa, wasomi na wanakwenda na kasi ya
upatikanaji wa taarifa hususan kupitia mitandao ya kijamii.
"Kutokana
na hilo mnao uwezo mkubwa wa kutushauri, kutujenga na kutukosoa,
tunakutegemeeni sana, toeni mawazo. mwaka huu tuna uchaguzi wa serikali
za mitaa, nawasihi vijana jitokezeni na gombeeni katika nafasi zote,"
alisema.
Kinana
alisema Chama kitafanya kila linalowezekena kuwapitisha vijana wengi
katika nafasi za kugombea kwani yeye na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan
watafanya kila jitihada kuwapitisha vijana wengi.
"Nawasihi
nendeni mkagombee nafasi zote na Chama tutatoa maelekezo kufanya
linalowezekena kuhakikisha vijana wanapewa nafasi nanyi hakikisheni
mnakipa ushindi Chama chenu," alisema.
Kinana alisema CCM ni kubwa, hivyo wanapaswa kukilinda, kujipanga, kuweka mikakati na kugawa majukumu.
Alisema
yapo mambo yanayochangia kukipa ushindi Chama ukiwemo utekelezaji mzuri
wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, hivyo aliwataka vijana kuchagua viongozi
wenye uwezo na sio wa kubebwa wala kutumia fedha kupata nafasi.
Hata hivyo, alisema Chama kisingependa kupata malalamiko bali kitachagua viongozi kulingana na sifa zao.
Kinana aliahidi kutoa kompyuta, mashine ya kuchapisha na ‘printa’ kwa vijana hao wajitegemee katika seneti yao.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abas Mtemvu
alisema ofisi ya Chama mkoa itachamgia sh. milioni mbili katika mfuko wa
vijana zitakazosaidia kununua vifaa mbalimbali ambavyo vitawawezesha
kujitegemea.
ZUNGU
Naibu
Spika wa Bunge, Mussa Zungu na Mbunge wa Ilala alisema wamepata
wananchama wapya, wasomi waliobobea zaidi ya 1,000 na wanatarajia
watayasemea mambo mazuri yanayotekelezwa na Rais Dk. Samia Suluhu
Hassan.
Alisema
hatua hiyo inaonyesha jinsi Rais Dk. Samia anavyofanya vizuri na
kugusa nyoyo za Watanzania, hivyo sasa Ilala wanaanza rasmi ajenda ya
Samia ya mwaka 2025 kuleta ushindi.
Alisema wameamua kumbeba na kumtetea kiongozi anayesimamia umoja wa Watanzania na kubeba kero zao.
"Msibabaishwe
wala msidanganywe na wasiokitakia mema Chama chetu na nchi yetu. Jimbo
la Ilala tutachangia sh. milioni tano mjisimamia na mikopo inayotewa na
serikali msizubae, ichangamkieni mjiimarishe," alisema.
MPOGOLO
Kwa
upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, alimpongeza
Kinana kwa kuwa mlezi mzuri wa vijana na jinsi anavyofanya kazi anawapa
nguvu ya kuendelea kuchapaka kazi.
Alisema
hali ya siasa kwa wilaya ya Ilala na Mkoa wa Dar es Salaam ni nzuri,
hivyo alishukuru na viongozi wa zuri wa Chama," alisema.
Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahman Kinana, akisalimia
Viongozi na Wanachama alipowasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu
Nyerere katika Mkutano wa Ukaribisho wa Wanachama 1170 wa Matawi ya
Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu katika Vyuo Vya CBE,DIT,IAE Mkoa wa Dar Es
Salaam.
V2
Wanachama
na Viongozi Mbalimbali wakiwa katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu
Nyerere katika Mkutano wa Ukaribisho wa Wanachama 1170 wa Matawi ya
Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu katika Vyuo Vya CBE,DIT,IAE Mkoa wa Dar Es
Salaam.
V3
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo akizungumza na Viongozi na
Wanachama katika Mkutano wa Ukaribisho wa Wanachama 1170 wa Matawi ya
Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu katika Vyuo Vya CBE,DIT,IAE
uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Mkoa wa
Dar Es Salaam.
v4
Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahman Kinana akikabidhi
kadi za CCM kwa Wanachama 1170 wa Matawi ya Seneti ya Vyuo na Vyuo
Vikuu katika Vyuo Vya CBE,DIT,IAE patika Mkutano uliofanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Mkoa wa Dar Es Salaam.
V5
Wanachama Wapya wakila Kiapo Cha Chama.
V6
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam Ndg. Abasi Mtemvu, akizungumza na Viongozi
na Wanachama katika Mkutano wa Ukaribisho wa Wanachama 1170 wa Matawi
ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu katika Vyuo Vya CBE,DIT,IAE
uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Mkoa wa
Dar Es Salaam.
V7
Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahman Kinana, akizungumza
na Viongozi na Wanachama katika Mkutano wa Ukaribisho wa Wanachama 1170
wa Matawi ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu katika Vyuo Vya CBE,DIT,IAE
uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Mkoa wa
Dar Es Salaam.(Picha na Fahadi Siraji wa CCM)





No comments:
Post a Comment