Madaktari
bingwa na bingwa bobezi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke (TRRH)
wamefanikisha kambi ya matibabu na uchunguzi, wakiwahudumia wagonjwa
577 na kufanya aina nne za upasuaji katika Kituo cha Afya Buza.
Kambi
hiyo iliyodumu kwa siku tano imejumuisha madaktari bingwa katika fani
mbalimbali za afya kama upasuaji, macho, kinywa na meno, mifupa,
utengamao, masiko, pua na koo (ENT), watoto, wanawake na uzazi, magonjwa
ya ndani, afya ya akili, pamoja na uchangiaji damu wa hiari. Matibabu
haya ya kibingwa yamefanyika katika wiki ya kuelekea siku ya kuzaliwa
kwa Mheshimiwa Raisi Dr Samia Suluhu Hassan, Raisi wa Jamhuri ya
Muungana wa Tanzania.
Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa Temeke, Dkt. Husna Msangi, Mratibu wa huduma za tiba,
amesema wakati wa kuhitimisha kambi hiyo kuwa kambi hiyo ni njia moja
wapo ya kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan za kutoa
huduma za kibingwa na bingwa bobezi kwa wananchi katika vituo vya afya.
Aidha,
ametoa wito kwa wananchi kutumia fursa za kambi kama hizo kwani
zinawapa nafasi ya kupata huduma za kibingwa kwa gharama zilezile za
kituo cha afya na hivyo kupunguza usumbufu wa kufuata huduma hizo katika
hospitali ya rufaa.
Dkt. Luti Chuwa, Mganga Mfawidhi wa Kituo
cha Afya Buza, ameshukuru Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke kwa ujio wa
madaktari bingwa hao na kusema kuwa kambi hiyo imenufaisha wakazi wa
kata ya Buza. Pia, amekaribisha tena madaktari bingwa kutoa huduma ili
kuboresha afya za wananchi.
Bw. Bakari Mdoe, mmoja wa wagonjwa
walionufaika na kambi hiyo, amefurahishwa na ujio wa madaktari bingwa
kutoka Temeke na kuwahimiza wananchi kutumia fursa kama hizo kupata
matibabu
January 26, 2024
Home
Unlabelled
MADAKTARI BINGWA KUTOKA HOSPITALI YA TEMEKE WAFIKIA WAGONJWA 577 BUZA
MADAKTARI BINGWA KUTOKA HOSPITALI YA TEMEKE WAFIKIA WAGONJWA 577 BUZA
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment