NA VICTOR MASANGU KIMARA
Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es
salaam (DAWASA) Ndugu Kiula Kingu ametembelea na kukagua miundombinu ya
maji iliyoathirika na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo
mbalimbali mkoani Dar es salaam na kuahidi maboresho yanafanyika usiku
na mchana ili kurudisha huduma maeneo yaliyoathirika.
Ndugu
Kiula ametembelea eneo la Kimara Michungwani darajani ambapo ambapo
uharibifu umetokea kwenye bomba la inchi 6, eneo la Bonyokwa Kijiweni
uharibifu umetokea kwenye bomba la inchi 8, eneo la Mbezi Magufuli
uharibifu umetokea kwenye bomba la inchi 6 na eneo la daraja la Gwajima -
Mivumoni uharibifu umetokea kwenye bomba la inchi 6 na kupelekea wakazi
wa maeneo hayo kukosa huduma.
Akizungumza
baada ya ukaguzi huo, Ndugu Kingu amesema athari iliyotokea kwenye
miundombinu ni kubwa na kupelekea baadhi ya maeneo kukosa huduma, lakini
DAWASA ipo kazini kuhakikisha huduma inaimarika.
"
Ni kweli tumepata changamoto ya miundombinu ya maji lakini kwa jukumu
tuliopewa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma, hivyo niwaombe radhi
wakazi wa Dar es salaam pia niwatoe hofu ya kuwa DAWASA tupo kazini
kuhakikisha huduma inarejea na kila eneo lililoathirika linafikiwa na
kufanyiwa maboresho" amesema Ndugu Kingu
Vilevile,
kwa upande wa miundombinu ya majitaka ameelezea kazi bado inaendelea ya
kuzibua maeneo ambayo yalipata changamoto ya kuziba baada ya kuingiwa
na mchanga pamoja na taka ngumu.
"
Kwa upande wa miundombinu ya majitaka mafundi wetu wapo kazini ambapo
wana vifaa vya kisasa wanaendelea na kazi ya kuzibua miundombinu,
tunaendela kuwaomba wananchi kuwa wavumilivu DAWASA tumejipanga
kuhakikisha hali inaimarika" amesema Ndugu Kiula.
No comments:
Post a Comment