HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 25, 2024

MWANGA UNAONEKANA SHIMO LA TAIFA STARS

HIERONIMUS GODFREY


AFCON ya mwaka huu Taifa stars imeonyesha nuru, kwa mara ya kwanza taifa la Tanzania tumekusanya walau point mbili ilikuwa Almanusuru tutinge 16 bora, kauli za tumekufa kiume zipo miongoni mwa watu wachache kwa sababu kila mmoja alisadiki inawezekana.

.


Salamu kutoka kuzima zimekuja wakati huu wa furaha kwa taifa stars, tukijinadi kwa kiwango tulichokionyesha dhidi ya Congo, salamu hizi si za heri bali ni za shari.

.

Afcon ya mwaka 2027 Tanzania ni miongoni mwa wenyeji wa michuano hii pendwa, lakini salamu za kutisha zinaisumbua akili yangu, mwaka 2027 taifa stars itakumbwa na anguko ambao huenda wote tulilitegemea.

.

Ni mwaka ambao mastaa wengi watatupa mkono wa kwaheri. mwaka 2027, Mbwana Samata atakuwa na miaka 34, Simon Msuva atakuwa na miaka 33, Himid mao miaka 34. Huku Mohamed Hussein, Mzamiru pamoja na Aishi Manula watakuwa na miaka 31.

.

kizazi kilichopigania bendera kwa jasho na damu kinakaribia kufika mwisho. Hofu yangu kubwa ni nani ataziba kikamilifu nafasi hizi, nani ataziba pengo la Simon msuva na Mbwana Samata? Nani atasimama golini na kutupa walau nusu ya ubora wa Aishi Manula?

.

Ukweli mchungu ni kuwa Tanzania tumeshindwa kuwa na project bora ya uzalishaji vipaji. Wapo wapi wale watoto waliochukua kombe la duniani la watoto wa mitaani mwaka 2014?

.

Hawakufika fainali kwa bahati mbaya, ushindi wa bao 6-1 dhidi ya marekani, 3-0 dhidi ya Argentina. 3-1 fainali dhidi ya Rwanda huku Frank William akifunga hat-trick fainali na golikipa Emmanuel kuibuka mchezaji bora wa mashindano. Haikuwa bahati mbaya bali ni vipaji halisi.

.

Huenda kizazi chao tungebahatika kupata Mbwana Samata mpya. Lakini kizazi chao kimeshasahaulika.

.

Wakati tukishuhudia mwisho wa kizazi chetu bora, ninatamani tungelikuwa na project za kutunza vipaji halisi. Ninakupenda Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Pages