HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 02, 2024

RIADHA TANZANIA YAKUNWA HOTUBA YA RAIS MWAKA MPYA

SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), limepongeza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan mkesha wa mwaka mpya, kwa kugusa sekta ya ya michezo hususan kutambua mchango mkubwa uliotolewa na wanariadha.



Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu RT, Wakili Jackson Ndaweka, hotuba ya Rais Dk. Samia, mbali ya kugusa sekta mbalimbali, hakuisahau michezo hususan Riadha kwa kuchangia mafanikio na kuitangaza vema Tanzania kimataifa kwa mwaka 2023.

"Sisi kama Riadha Tanzania tumeguswa sana na hotuba ya Mheshimiwa Rais, hususan tumefarijika sana pale alipotambua mafanikio ya wanariadha wetu Magdalena Shauri na Alphonce Simbu," alisema Wakili Ndaweka na kuongeza:

Hii itachochea kujituma zaidi na kufanya vizuri kwa vijana wetu na sisi kama shirikisho tunaahidi kujituma na kujipanga zaidi kwa kushirikiana na Serikali hususan Wizara yenye dhamana na michezo, wadhamini na wadau mbalimbali ili kuleta mafanikio makubwa zaidi katika medani ya Riadha.

Katika hotuba take, Rais Dk. Samia akielezea mafanikio katika sekta ya michezo alisema:

"Kwenye sekta ya michezo, pamoja na kuimarisha miundombinu ikiwamo ukarabati Uwanja wa Benjamin Mkapa, mwaka huu tumepata mafanikio mengi ya kujivunia ikiwemo:

Timu ya Yanga kupata medali ya pili kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika 'CAF Confederation Cup' na:

Binti wa Kitanzania Magdalena Shauri kuwa mshindi wa tatu kwenye mbio za Berlin Marathon na mwanariadha Alphonce Simbu kuwa mshindi wa pili kwenye mbio za  Shanghai Marathon.

No comments:

Post a Comment

Pages