HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 05, 2024

Wadau wakutana kujadili namna ya kupambana na upungufu wa lishe

Katika kuhakikisha matatizo ya ukosefu wa lishe unaowakabili binadamu wakiwemo mama wajawazito ambao upelekea kuzaa watoto wa vichwa vikubwa na mgongo wazi unatoweka, Serikali imejipanga kuongeza virutubisho vya vitamini na madini kwenye vyakula ambavyo vitasadia kuimarisha kinga ya mwili.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma  na Mtafiti na mratibu wa shughuli za uongezaji virutubisho kitaifa, Selestine Mgoba wakati alipokuwa kwenye warsha ya kutekeleza maagizo ya viongozi juu ya kupambana na upungufu wa lishe iliyoandaliwa na Wizara ya Viwanda na Biashara na kuwakutanisha wanakamati kutoka wizara mbalimbali na Sekta binafsi.

Amesema kuwa kutokana na  matatizo hayo wamechagua vyakula vikuu ambavyo ni unga wa ngano,unga wa mahindi,mafuta ya kula na chumvi ambavyo vitaongezwa madini ya chuma ambavyo vitaimarisha kinga ya mwili na kwa akina mama kuwa msaada.

"Tunaona kwenye Taifa letu upungufu wa Damu ambayo usababishwa na upungufu wa madini chumvi zaidi ya asilimia 59 ya watoto wa kitanzania chini ya umri wa miaka mitano wana upungufu wa Damu kwa hiyo wazalishaji wakiwa na utaratibu wa kuongeza madini chumvi kwenye vyakula  tulivyo vibainisha" amesema Mtafiti Mgoba.

Aidha Mgoba  amesema katika kuboresha lishe nchini tayari kuna kiwanda ambacho kitarahisisha wananchi kupata virutubisho kwa wakati tofauti na hapo awali ambavyo ilitakiwa kuagiza nje ya nchi.

Nae Kaimu Mkurugenzi idara ya  viwanda vidogo na Biashara ndogo  ,Wizara ya Viwanda na Biashara Mhandisi Ilege Charles amesema kuwa wazalishaji wengi wa vyakula ni wadogo ambao jukumu kubwa ni kuwasimamia na kuwapa elimu namna ya kuchakata na kuzalisha virutubisho.

"Sisi Idara ya Viwanda na Biashara ni kusimamia wajasiliamali wanachakata vyakula kwa hali ya viwango na kwa kushirikiana na halmashauri zetu nchini tumejipanga kutoa elimu mambo ya lishe kwa jamii ili ielewe kwa nini tunasema tuongeze virutubisho ili kuondoa matatizo na watoto wa migongo wazi na vichwa vikubwa. "Amesema Mhandisi Charles.


Kwa upande wake Afisa Lishe mwandamizi Peter Kaja kutoka Wizara ya Afya amesema Takwimu za mwaka 2022 zinaonesha hali ya udumavu nchini  imefika asilimia 30 kutoka asilimia 31 licha ya kwamba zipo baadhi ya mikoa ipo mpaka asilimia 56 na lengo la nchi ni kufikia asilimia 20 ya udumavu.

" Inapaswa kupambana na akina mama wajawazito kuwapatia madini Chuma ili kusaidia afya zao na serikali imepambana kupunguza vifo vya wazazi kutoka 500 mpaka kufikia 400 hivyo wakitumia madini chuma itasaidia kupambana na tatizo hilo wakati wa kujifungua" amesema Afsa lishe Kaja.

Nae Mwanasheria Wizara ya Viwanda na Biashara Jonas Mujungu amesema kanuni za wizara  zimetungwa kwa ajili ya kupambana na changamoto za kile ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM)inayowataka wizara za kisekta na wadau mbalimbali watafute afua za kupambana na changamoto za lishe hapa nchini.

Mujungu ameeleza kuwa katika kutekeleza kanuni hizo ambazo zinawaruhusu watu wanaotaka kurutubisha kwa ihari kwa kupata mwongozo wa Tbs hususani vyakula vinne ambavyo vinatumiwa na watu wengi ambavyo ni unga wa ngano, unga wa mahindi, chumvi na mafuta ya kula.

Tumsime Nkyando ni mshiriki kutoka Shirika la Kimataifa  lisilo kuwa la kiserikali Tekno self linalofanya kazi na jamii zinazoendelea kujenga uchumi wao na Biashara  amesema kuwa suala la lishe ni moja ya maeneo wanayoyalenga .

Kuwa Kanuni iliyojadiliwa italeta tija kubwa katika kujenga afya njema kwani wasipokuwa na lishe inaweza kupelekea kutokuwa na uwezo mkubwa wa kimaamuzi na kufikiria zaidi.

No comments:

Post a Comment

Pages