Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Kushoto), akimkabidhi mwongozo wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya 438 kwa Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi, Bw. Robert Manyama, baada ya kuzindua Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (Tax Ombudsman Service Tanzania - TOST), katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi ni chombo huru chenye jukumu la kupitia na kushughulikia malalamiko yote ya walipakodi kuhusu huduma, masuala ya kiutaratibu na kiutawala yanayoweza kujitokeza katika usimamizi wa sheria za kodi zinazotekelezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA.
Na Farida Ramadhani, WF-Dodoma
Waziri
wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) ameiagiza Ofisi ya
Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za kodi (TOST) kuhakikisha inatatua
migogoro mbalimbali ya kodi kwa wakati ili kuiwezesha Serikali kukusanya
mapato pamoja na kuimarisha mazingira ya ufanyaji biashara nchini.
Dkt. Nchemba alitoa agizo hilo Jijini Dodoma wakati akizindua rasmi Ofisi hiyo mpya ambayo iko chini ya Wizara ya Fedha.
Mhe.
Nchemba alisema kuwa Serikali inatarajia kwamba Ofisi hiyo itasaidia
kupunguza migogoro ya kikodi na kuongeza kiwango cha ulipaji kodi kwa
hiari, hivyo kuongeza mapato ya Serikali.
“Ofisi
hii utasaidie kupunguza migogoro ya kodi na kuongeza kiwango cha
ulipaji kodi kwa hiari, siku tukifanikiwa kuongeza idadi ya walipakodi
(taxbase), tutakuwa na uhuru mkubwa sana wa kupunguza hivi viwango vya
ulipaji kodi”, alisema Mhe. Dkt. Nchemba.
Alisema
ni matarajio ya Serikali kuwa ustawi wa biashara utaongezeka kutokana
na walipa kodi kupata jukwaa huru litakalotoa fursa ya kusikiliza
changamoto zinazohusu usimamizi wa sheria ya kodi pamoja na huduma
zinazotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Mhe.
Dkt. Alisema Wizara ya Fedha itaendelea kusimamia na kuboresha utendaji
wa Taasisi hiyo kwa kuhakikisha kuwa mahitaji yote muhimu yanapatikana
ikiwemo rasilimali watu, vifaa na mifumo ya kisasa ili iweze kutoa
huduma bora kwa walipa kodi.
Aidha,
Aliagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea kukusanya kodi kwa
weledi kwa kutafuta njia ya majadiliano na wafanyabiashara wanaokiuka
taratibu badala ya kufunga biashara zao.
Mhe.
Dkt. Nchemba aliwaagiza Wafanayabiashara kufanya biashara zao kwa
kufuata sheria, taratibu na kanuni zilizopo ili kuepusha misuguano isiyo
ya lazima na Mamlaka ya Mapato.
Pia
alitoa rai kwa wananchi kuwa wazalendo kwa kulipa kodi stahiki na kwa
wakati, kudai risiti halali kulingana na kiwango cha fedha walichotoa na
wafanyabiashara kufanya matumizi sahihi ya mshine za kutolea risiti kwa
njia ya kielekroniki (EFDs) pamoja na kutoa risti halali kwa wateja
wao.
“Watu
wanaostahili kutumia mashine za EFDs watumie, kutokufanya hivyo ni
kujitafutia matatizo wenyewe. Kutokutoa risiti na kusingizia mifumo sio
suluhisho la kudumu, huku ni kuahirisha matatizo” alisitiza Mhe. Dkt.
Nchemba.
Alisema
kufanya hivyo, kutaiwezesha Serikali kutoa huduma muhimu za kijamii
ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali itakayoboresha
maisha yao na kupunguza umasikini ikiwemo maji, elimu, miundombinu
wezeshi kiuchumi na mambo mengine mengi.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Taasisi ya Usuhulishi wa Malalamiko na Taarifa za
Kodi (TOST), Bw. Robert Manyama alisema kuwa Taasisi yake imejipanga
kutatua changamoto za taarifa za kikodi za wananchi katika ubora wa hali
ya juu kwa kuwa imeweka mazingira rafiki na rahisi ya wananchi
kuwasilisha malalamiko yao popote walipo pamoja na kuwa na wafanyakazi
wenye ueledi na waliotayari kutoa huduma kwa walipa kodi.
“Kipaumbele
cha Ofisi hii ni kuhakikisha kwamba malalamiko yote yanashughulikiwa
kwa uhuru kamili, haraka, haki na usawa”, alibainisha.
Alisema
Ofisi hiyo imeanzishwa kutokana na marekebisho ya Sheria ya Fedha namba
8 ya mwaka 2019, yaliyosababisha marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa
Kodi SURA 438, kwa kuongeza sehemu ya IIIA – Uanzishaji wa Ofisi ya
Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (Establishment of Tax
Ombudsman office.)
Bw.
Manyama alisema marekebisho ya sheria yaliipatia Ofisi hiyo jukumu
mahususi la kupokea, kusajili na kusuluhisha Malalamiko yatokanayo na
usimamizi wa sheria za kodi ili kuyapunguza na kutoa mapendekezo ya
maboresho ya mfumo wa ukusanyaji kodi nchini pamoja na kuongeza ulipaji
kodi wa hiari na kupunguza gharama za ukusanyaji wa kodi ya Serikali.
Naye
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Daniel Baran
Sillo (Mb), alisema Kamati hiyo imependekeza Ofisi ya Msuluhishi wa
Malalamiko na Taarifa za Kodi kuhakikisha inajulikana kwa wadau wote wa
kodi nchini na itekeleze majukumu yake kikamilifu ya kutatua changamoto
za walipakodi.
Alisema
Kamati pia imependekeza Ofisi hiyo kuendelea kushauri namna ya kutatua
changamo ya mifumo ya kodi nchini iliyosababisha migogoro na kuifanyia
marekebisho mifumo husika.
Mhe.
Sillo aliishauri Ofisi hiyo iendelee kufanyia kazi changamoto za kikodi
zinazojirudia na kutafuta suluhisho la kudumu huku akitolea mfano wa
tatizo la utoaji na uombaji risiti.
Aidha,
Kamati ilipendekeza Serikali, kupitia Taasisi hiyo, itafute mfumo wa
kielektroniki utakaotumika kupokea malalamiko, kuyashughulikia na kutoa
mrejesho huku kwa wadau na kusisitiza kuwepo uwazi katika utekelezaji wa
majukumu yao.
No comments:
Post a Comment