Dar
es Salaam 19 February 2024 – Katika jitihada za kuendeleza sekta ya
habari nchini, Benki ya CRDB imeendesha semina maalum kwa wadau wa sekta
ya habari nchini na uchumi “CRDB Bank Media Day” iliyofanyika katika
Makao Makuu ya benki hiyo yaliyopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
Akifungua
semina hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela
amesema “CRDB Bank Media Day” ya mwaka huu imejikita katika kuangazia
ripoti ya Finscope 2023 na namna gani vyombo vya habari vinaweza
kuchochea ujumuishi nchini.
“Ripoti
ya Finscope ya 2023 inaonyesha ujumuishi wa kibenki upande wa huduma za
benki ni 22% tu pamoja na jitihada na ubunifu mkubwa katika bidhaa. Hii
inaonyesha kuna ombwe kubwa la elimu ya fedha, hivyo leo tumepata
kujadili ninamna gani wenzetu wa sekta ya Habari wataweza kusaidia kutoa
taarifa na huduma za fedha,” alisema Nsekela.
Katika
semina hiyo waandishi wa habari walipata fursa ya kupata mafunzo ya
namna ya bora ya kaandaa na kutoa mafunzo ya taarifa za biashara, fedha
na uchumi. Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB na Mkurugenzi
Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa amesema mafunzo
hayo ni sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kusaidia kujenga
waandishi mahiri nchini.
Akizungumza
katika semina hiyo, Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi
ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuandaa semina hiyo iliyowaleta wadau wa
sekta ya habari kujadili namna ya kuongeza mchango wake katika maendeleo
hususani katika kuongeza ujumuishi wa kifedha nchini. Matinyi
amewahakikishia wadau wa sekta hiyo kuwa Serikali itaendelea kuweka
mazingira mazuri yatakayosaidia kuboresha sekta ya habari.
Mada
mbalimbali zimewasilishwa katika semina hiyo ikiwamo ‘Jukumu la Vyombo
vya Habari katika kuchochea Ujumuishi wa Kifedha’ iliyowasilishwa na
Mhariri Mstaafu wa Nationa Media Group Kenya, Charles Onyango Obbo,
‘Elimu ya Fedha kupitia Mitandao ya Jamii’ iliyowasilishwa na Fayness
Sichwale amshauri wa masuala binafsi ya fedha na Mwanzilishi wa Personal
Finance Hub, na Usomaji na Uwasilishaji wa Taarifa za Fedha’
iliyowasilishwa na Dkt. Ndalahwa Masanja, Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu
cha ESAMI.
Katika
Semina hiyo iliyohudhuriwa na waandishi na wahariri kutoka vyombo mbali
nchini, Benki ya CRDB pia imezindua shindano maalum la kutafuta
waandishi wahabari wachanga wa habari za biashara, fedha, na uchumi.
Shindano hilo ambalo litaendeshwa kwa muda wa miezi miwili hadi Aprili
12 2024, litatoa washindi watatu ambao watajishindia zawadi ya Sh.
Milioni 1 na nafasi ya kufanya kazi na Benki ya CRDB.
Aidha,
katika hafla hiyo Benki ya CRDB imetoa tuzo za kutambua mchango wa
waandishi wa habari wawili nguli katika sekta ya habari nchini.
Waliokabidhiwa tuzo hizo ni Edda Sanga mwandishi mstaafu wa Shirika la
Habari la Tanzania (TBC) na Mwenyekiti wa Umoja wa Waandishi wa Habri
Wanawake (TAMWA), na Ndimara Tegambwage mwandishi wa zamani wa magazeti
ya Uhuru na Mzalendo, na moja ya waanzilishi wa Taasisi ya Vyombo vya
Habari Kusini mwa Afrika (MISA).
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO,
Mobhare Matinyi, akimkaidhi Tuzo ya Heshima kutoka Benki ya CRDB kwa
Mwanahabari wa Habari Mkongwe nchini, Mzee Ndimara Tegambwage , ikiwa
sehemu ya kutambua mchango wake katika tasnia ya Habari hapa nchini,
wakati wa semina maalum kwa wadau wa sekta ya Habari za uchumi nchini
iliyoandaliwa na Benki va CRDB na kutamuliwa kama "CRDB Bank Media Day"
ilivofanyika katika Makao Makuu ya benki hive yalivopo barabara ya Ali
Hassan Mwinyi, jijini Dar es salaam. Wengine pichani kutoka kulia ni
Mkurugenzi Mtendaii wa Benki va CRDB, Abdulmajid Nsekela, Afisa Mkuu wa
Uendeshaji wa Benki va CRDB Bruce Mwile pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa
CRDB Bank Foundation na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki va CRDB,
Tully Esther Mwambapa.
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO,
Mobhare Matinyi, akimkaidhi Tuzo ya Heshima kutoka Benki ya CRDB kwa
Mwanahabari wa Habari Mkongwe nchini Mama Eda Sanga, ikiwa sehemu ya
kutambua mchango wake katika tasnia ya Habari hapa nchini, wakati wa
semina maalum kwa wadau wa sekta ya Habari za uchumi nchini
iliyoandaliwa na Benki va CRDB na kutamuliwa kama "CRDB Bank Media Day"
ilivofanyika katika Makao Makuu ya benki hive yalivopo barabara ya Ali
Hassan Mwinyi, jijini Dar es salaam. Wengine pichani kutoka kulia ni
Mkurugenzi Mtendaii wa Benki va CRDB, Abdulmajid Nsekela, Afisa Mkuu wa
Uendeshaji wa Benki va CRDB Bruce Mwile pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa
CRDB Bank Foundation na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki va CRDB,
Tully Esther Mwambapa.
Mkurugenzi Mtendaji wa
CRDB Bank Foundation na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki va CRDB,
Tully Esther Mwambapa akizunguma katika semina maalum kwa wadau wa sekta ya Habari za uchumi nchini
iliyoandaliwa na Benki va CRDB na kutamuliwa kama "CRDB Bank Media Day"
ilivofanyika katika Makao Makuu ya benki hive yalivopo barabara ya Ali
Hassan Mwinyi, jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment