NA VICTOR MASANGU, CHALINZE
HALMASHAURI
ya Chalinze Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani hatimaye imepitisha
mapendekezo ya bajeti ya kiasi cha shilingi bilioni 54.6 kwa kipindi cha
mwaka wa fedha wa 2024/2025.
Hayo
yamebainishwa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Chalinze
Ramadhani Possi wakati wa kikao maalumu cha baraza la madiwani kwa
ajili ya kujadili na kupitisha mapendekezo ya bajeti.
Possi
alibainishwa kwamba bajeti hiyo ambayo imeweza kugusa katika nyanja
mbali mbali imepitia vikao mbali mbali vya kisheria pamoja na
kuwahusisha madiwani kutoka kila kata kwa lengo keleta maendeleo.
Mkurugenzi
huyo alifafanua kwamba katika mapendekezo ya bajeti hiyo fedha za
ndani zitakuwa ni shilingi bilioni 17.3 luzuku kutoka serikalini kuu na
matumizi ya kawaida ni bilioni 26.01.
"Mwenyekiti
ninaomba baraza lako tukufu lipitishe mapendekezo ya bajeti hii ya
bilioni 54.6 na kwamba itajumusha na mambo ya mishahara miradi ya
maendeleo pamoja na mahitaji mengine ya kiofisi,"alifafanua Possi.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Mhe.Hassan
Mwinyikondo amewapongeza wataalamu pamoja na madiwani wote kwa kuweza
kushirikiana kwa pamoja katika kuandaa mapendekezo ya bajeti hiyo.
Alisema
kwamba kwamba hawezi kusita kuisifia bajeti hiyo kutokana na kuweza
kugusa katika kila nyanja pamoja na kutoa fursa za maoni na mapendekezo
ambayo yalikuwa yanatolewa kwa maslahi ya wanannchi.
"Kiukweli
hii bajeti yetu imeweza kugusa kila nyanja maana siku zote sisi
madiwani kwa kushirikiana na madiwani tumekaa kuanzia asubuhi mpaka
jioni nia na madhumuni kuyachukua mapendekezo yote ambayo yametolewa na
kuyaingiza katika bajeti,",alisema Mwinyikondo.
Pia
alisema kuwa bajeti hiyo itakwenda kuleta chachu kubwa ya mabadiliko
katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo itakuwa ni
faida kubwa kwa wananchi wa chalinze.
Mwenyekiti
huyo aliongeza kubwa lengo kubwa la kupendekeza bajeti hiyo ni
kuhakikisha inakwenda kuokoa maisha ya wananchi wa chalinze pamoja na
kuibua miradi mipya ya maendeleo.
"Waandishi
wa habari nadhani mnajionea nyinyi wenyewe kwa hivyo yale mazuri yote
ambayo tunayatekeleza ni vema mkayaandika kutokana na mambo mazuri
ambayo tunayatekeleza,"alisema Mwinyikondo.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Halima Okash hakusita kuipongeza Halmashauri
ya Chalinze kwa juhudi zake katika kutekeleza miradi mbali mbali ya
maendeleo.
Mkuu huyo
alisema amefarijika kuona madiwani na wataalamu mbali mbali wanafanya
kazi kwa pamoja katika kuhakikisha kwamba wanaweka mipango ya kutekeleza
miradi ya maendeleo kupitia fedha za ndani.
Alisema
mapendekezo ya bajeti hiyo yanatakiwa kusimamiwa ipasavyo ikiwa
sambamba na kumsaidia Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan ili
aweze kutimiza majukumu yake ipasavyo.
Nao
baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Chalinze wameungana kwa pamoja
kupitisha mapendekezo ya bajeti hiyo ambayo wamesema itakuwa ni mkombozi
mkubwa kwa wananchi katika sekta mbali mbali.
No comments:
Post a Comment