NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Viongozi
wa chama cha mapinduzi (CCM) wametakiwa kuachana kabisa na tabia ya
kulalamika kwa kutumia mitandao ya kijamii na badala yake wanatakiwa
kuzingatia vikao halali vya kikanuni au kumtafuta muhusika ili kupata
ufumbuzi.
Kauli hiyo
imetolewa na Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha Mjini
Issack Kalleiya wakati wa kikao kazi kilichofanyika Katika Ukumbi wa
CCM Wilaya na kuwakutanisha madiwani wa kata zote 14 za Kibaha Mjini na
Wenyeviti wa Serikali za Mitaa.
Katibu
huyo alisema kuwa viongozi wanapaswa kutimiza wajibu wake ipasavyo kwa
kufuata maelekezo ya chama kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa
na sio vinginevyo kulalamika kwenye mitandao ya kijamii.
Katibu
huyo alisema kwamba viongozi CCM wanatakiwa wajiweke tayari kwa
uchaguzi na kuacha kulalamika kwa watu ambapo jambo hilo limekua
linashika kasi kwa baadhi ya viongozi kutoa siri za vikao na kuwapa watu
ambao hawahusiki.
Katibu
wa CCM amesisitiza kuwa kwa sasa Wilaya ya Kibaha Mjini ina jambo kubwa
la Uchaguzi ww Udiwani Kata ua Msangani hivyo amewataka wote kujiweka
tayari kwa kushiriki katika Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Machi
20,2024.
Aidha, Katibu
Kalleiya amewataka Madiwani pamoja na wenyeviti wa Serikali za Mitaa
kushiriki katika Uchaguzi wa Udiwani Kata ya Msangani pindi
watakapohitajika ikiwemo kusaidia kunadi Chama wakati wa kampeni na
kutafuta kura kwa wananchi ili CCM ishinde kwa kishindo.
Katibu
Wa CCM amesema, wote wanatakiwa wawe tayari ambapo ratiba ya uchukuaji
na urudishani wa fomu za Uchaguzi unaanza tarehe 21/02/2024 hadi
23/01/2024.
Naye
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha na Diwani wa Kata ya Sofu Mhe.
Mussa Ndomba amepokea maelekzo hayo kwa kuahidi kushirikiana na Chama
katika Uchaguzi huu mdogo wa marudio ili kuhakikisha CCM inashinda kwa
kishindo.
Pia, amesema
maelekezo yote yaliyotolewa watayafanyia kazi na kwa sasa watakuwa
wanakaa vikao pamoja katika ya madiwani na wenyeviti wa Serikali za
Mitaa sambamba na Mkurugenzi ili kujadili masuala mbalimbali na kuweza
kutatua changamoto zilizopo katika mitaa yao.
Kikao
hicho kilitoka na kauli moja ya CCM Moja KIbaha Moja ambapo wote
Madiwani na Wenyeviti walikubali kushirikiana katika kukijenga Chama,
kusimamia na kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
No comments:
Post a Comment