Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Balozi Dkt. Emmanuel John
Nchimbi, akitia saini kitabu cha maombolezo wakati wa kutoa heshima za
mwisho na kuaga mwili wa marehemu Luteni Jenerali (mstaafu) Balozi
Martin Nikusubula Mwakalindile, katika Hospitali Kuu ya Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo, jijini Dar Es Salaam, Februari 2,
2024.
.jpeg)
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwapatia mkono wa pole familia ya Luteni Jenerali (mstaafu) Balozi Martin Nikusubula Mwakalindile wakati wa shughuli ya kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa marehemu Luteni Jenerali Mwakalindile, iliyofanyika katika Hospitali Kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo, jijini Dar Es Salaam, Ijumaa Februari 2, 2024.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akitoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa marehemu Luteni Jenerali (mstaafu) Balozi Martin Nikusubula Mwakalindile, katika Hospitali Kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo, jijini Dar Es Salaam, Ijumaa Februari 2, 2024.
Rais Mstaafu, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Jacob John Mkunda wakati kiongozi huyo alipoongoza waombolezaji wengine kushiriki shughuli ya kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa marehemu Luteni Jenerali (mstaafu), Balozi Martin Nikusubula Mwakalindile, iliyofanyika Hospitali Kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), leo Ijumaa, Februari 2, 2024. Kulia katika picha ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Stergomena Lawrence Tax na kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi.



.jpeg)
.jpeg)



No comments:
Post a Comment