HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 18, 2024

NMB Yakabidhi Madawati, Mabati kwa Shule za Wilaya ya Rorya

Mkuu wa Wilaya ya Rorya mkoani Mara Juma Chikoka (kushoto) akipokea sehemu ya msaada wa madawati 150 kwa ajili ya Shule ya Msingi Minigo kutoka kwa Kaimu Meneja wa NMB kanda ya Ziwa Hamadan Silliah, ambapo NMB pia imetoa madawa 100 kwa shule ya Msingi Nyanduru,mabati 168 kwa shule ya Girango,mabati 100 kwa Shule ya Sekondari Prof Sarungi  na ukarabati wa madarasa 7 ya shule ya msingi Minigo, msaada wote una jumla ya Sh 84 milioni.

 

Na Mwandishi Wetu

 

BENKI ya NMB imetoa msaada wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 80 ukiwa ni madawati 250 pamoja na mabati 368 kwa shule tano za Halmashauri ya Wilaya ya Rorya mkoani Mara. Shule zilizonufaika na msaada huo ni Shule ya Msingi Minigo ilipata madawati 100, shule ya msingi ya msingi Nyanduru madawati 100. 

 

Shule zilizopokea mabati ni shule ya msingi Gilango iliyopokea mabati 168. Shule ya msingi Kiamwani imepokea mabati 100, mbao pamoja na misumari. Shule ya sekondari Profesa Philemon Sarungi imejengewa hosteli mbili na kupewa shilingi milioni 15.

 

Mbali na misaada hiyo, benki hiyo pia imefanya ukarabati wa madarasa saba katika shule ya msingi Minigo pamoja na kumalizia ujenzi wa darasa moja katika shule hiyo.

 

Akizunguzmza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika jana katika shule ya msingi Minigo,  Mkuu wa Wilaya ya Rorya Juma Chikoka ameishukuru sana benki ya NMB kwa kuweza kusaidia uboreshaji  wa miundo mbinu ya elimu katika wilaya ya Rorya. Chikoka alikiri kuwa wilaya ya Rorya inakabiliwa na changamoto kubwa sana ya uchakavu wa miundo mbinu ya elimu.

 

"Misaada mbalimbali ya elimu tunayopokea kutoka NMB imeweza kuzisaidia shule zetu tatu za sekondari katika Wilaya ya Rorya zimeingia katika kumi bora ya mkoa wa Mara katika mitihani ya taifa(NECTA) ya kidato cha nne " amesema.

 

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya ameiomba benki ya NMB kufikiria kuwa mdhamini wa Tuzo za elimu katika wilaya ya Rorya zenye lengo la kusaidia shule ziweze kufanya vizuri katika mitihani ya kitaifa.

 

Katika hatua nyingine,Chikoka ameiomba benki ya NMB iwasaidie kutoa mikopo ya wavuvi ili waweze kutumia ufugaji wa Vizimba  na mikopo kwa wakulima waweze kutumia kilimo cha umwagiliaji.

 

Naye Kaimu meneja wa benki ya NMB Kanda ya Ziwa Hamadan Sillia amesema benki yao itaendelea kusaidia jamii kwani kushiriki katika kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili jamii wanazohudumia ni moja ya kipaumbele cha Benki hiyo.

 

“Ni faraja kwa Benki ya NMB kuona tunashirikishwa katika masuala muhimu kama utatuzi wa changamoto zinazoikabili jamii yetu, hii inaonesha ni namna gani mnaitambua Benki ya NMB kama sehemu ya jamii zenu, ni heshima na tunashukuru sana,” alisema Bw. Hamadan

 

Wakati huo pia, Kaimu Meneja wa Kanda ambae pia ni Meneja wa Benki hiyo tawi la Kenyata Rod Jijini Mwanza Amewaomba walimu na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya kuendelea kutumia huduma mbalimbali za Benki ya NMB ikiwemo ufunguaji wa Akaunti za NMB Pesa ambazo hufunguliwa kwa shilingi 1000 tu.

 

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Minigo, Mwalimu Joseph Onyango amesema benki ya NMB imewasaidia kuongeza maudhurio ya wanafunzi kutokana na uboreshaji wa madarasa na wanategemea pia ongezeko la ufaulu..

No comments:

Post a Comment

Pages