Msanii Ben Paul akitumbuiza kwenye sherehe ya Saadan Aura.
Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Hifadhi ya Taifa imewataka Watanzania kujitokeza kutembelea vivutio vya utalii ili kuongeza mapato ya ndani.
Wito huo umetolewa na Kamanda wa Uhifadhi wa Kanda ya Mashariki, Gibril Mwishawa, (Februari 25, 2024), ambapo amewataka kuwa na utamaduni wa kutembelea hifadhi zilizopo nchini.
Mwishawa alisema Tanzania ina utajiri wa hifadhi na Tanapa wana Kanda nne za kiutawala kwa Kanda ya Mashariki ambazo ni Saadan, Nyerere, Mikumi na Udizungwa.
Akizungumza kuhusu hifadhi ya Sadaan ambapo wamefanya Tamasha la kuhamasisha utalii lililopewa jina la Aura 2024, alisema hifadhi hiyo ni muhimu kwa sababu ya kuwa na vionjo vya mbuga na bahari.
Alitaja sababu nyingine ya Watanzania kutembelea hifadhi hiyo kuwa ni kuchangiwa na kutembelewa sana na watalii na wageni, kama ilivyo kwa zile za Kaskazini.
Katika kuhakikisha hilo linakamilika amesema tayari wameshaainisha maeneo ya uwekezaji na yameshatumwa maombi mbalimbali ikiwemo na hifadhi ya Saadan kwa lengo la kusaidia kukuza utalii katika Hifadhi za Kanda za Mashariki.
Naye Kamishna msaidizi wa Maendeleo ya biashara Tanapa Jully Lyimo, akizungumzia kuhusu Sadaan alisema ni eneo zuri kwakuwa lina vivutio vya utalii wa kupanda gari, kuona wanyama, utalii wa kutembea, utalii wa usiku, utalii wa fukwe na boti.
Lyimo alitoa wito kwa Watanzania kutumia hifadhi hiyo ya Saadan, kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kipaimala, harusi na sherehe nyingine.
No comments:
Post a Comment