HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 04, 2024

R.I.P "KICHWA CHA MWENDAWAZIMU"

Na John Richard Marwa


Ameondoka shujaa na Rais wa awamu ya pili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi. Ameondoka Mzee wa Ruksa, Bendera Nusu mlingoti si pwani wala visiwani sio Bara wala Pemba kote nchi imezizima.



Wakati Taifa likiwa kwenye majonzi mazito, Watanzania wako kwenye kilele cha mafanikio makubwa ya mchezo wa Soka ambao Hayati aliwahi kusema ni kichwa cha  mwendawazimu miaka ya 1993. Wakati mwili wake ukiingia kaburini Bendera ya Tanzania licha ya kupepea nusu mlingoti nchini, Afrika imepepea kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro.


Tokea kuumbwa kwa misingi ya Ulimwengu kwa mara ya kwanza Tanzania imeingiza timu mbili hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL. Yanga kutoka kundi D na Mnyama kutoka kundi B.


Shughuli ilikamilishwa jana na wale waliosababisha Hayati kuitaja nchi hii ni kichwa cha mwendawazimu kwenye medani za Soka ambapo Simba walipoteza Kombe la CAF dhidi ya Stella Abidjan kwa mabao mawili kwa bila Uwanja wa Taifa Sasa Uhuru baada ya kutoka Suluhu ugenini  mchezo wa kwanza.


Yawezekana imehitajika miaka 31 kufutika kwa kauli ya Hayati ikiwa hayuko tena Duniani kimwili ama kuna kazi ya kufanyika zaidi hasa kwa Simba na Yanga katika hatua ya Robo Fainali??


Kuna mambo sita yametokea wakati Hayati anapumzishwa  kwenye makazi ya milele, Mosi ni salamu za pole kutoka Bujumbura Burundi kwa watanzania kupitia kwa Saido Ntibanzonkiza dakika ya Saba ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL Simba dhidi ya Jwaneng Galaxy Benjamin Mkapa.


Jambo la pili ni salamu kutoka ma Rasta Falai wa muziki wa Rege wote Duniani enzi za utawala wa Hayati ulikuwa miongoni mwa muziki pendwa, Kibu Denis akaweka msumari wa pili.


Dakika ya 22 Par Omar Jobe, akatia msumari wa tatu kwa niaba ya watalii wote Bara la Afrika ndani ya ardhi ya Mama Samia akaweka shada.


Haikuwa ajizi kwa mtakatifu wa Soka la Tanzania na mchezaji bora wa muda wote kuwahi kutokea ikawa Ruksa kwake kumuaga Mzee wa Ruksa pia ni salamu za polee za wajukuu wa Mzee Kaunda kutoka Zambia kwenda Zanzibar zikafikiswa na The Brain 🧠.


Wajukuu nao tukawakilishwa na kijana maridadi kuweka shada la maua kwenye kaburi la Hayati, mchezo wa kwanza, siku ya kwanza, Ladack Chasambi, touch yake Ligi ya Mabingwa Afrika akaweka chuma cha tano.


Jambo la sita, Wacongo wao ni akina nani hata wasimzike Hayati? Fabrice Luamba Ngoma akaweka chuma cha sita na kuwaambia watanzania hatutasita kamwe kumuenzi Mzee wa Ruksa Bendera Nusu mlingoti Afrika imepepea kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro twenzetu Robo Fainali na hii ndio Namba sita za Airport.


Kama ambavyo Taifa hili miaka na mikaka halitaacha wala kusahau Wazee wetu waliotangulia mbele za haki ndivyo ambavyo jina la CHAMA halitasaulika wala kufutika katika vitabu vya historia ya Soka la Tanzania milele.


Ni mjukuu wa Mzee Kaunda bahati mbaya yuko Msimbazi na heshima yake hata pale Kaunda inaeleweka na inaheshimika.


Pumzika kwa Amani Mzee wa Ruksa, Tanzania iko salama na Soka liko salama mikononi mwa Wallace Karia pale Karume. R? #€,

 //0

Hongera Mnyama hongera Wananchi tukutane Nusu ama Fainali ya CAF CL 2023/24


✍️@MasterPlan

No comments:

Post a Comment

Pages