HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 19, 2024

BENKI YA AKIBA YAZINDUA RASMI HUDUMA YA KADI ZA VISA



Na Magrethy Katengu


Benki ya Akiba (ACB) imezindua rasmi huduma ya kadi za VISA ambazo ni mahususi kwa kufanya huduma za miala ya kifedha  ambapo inauwezo wa kutumika sehemu yoyote Duniani.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo wa ACB VISA, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Silvest Arumasi amesema kwamba Benki ya ACB inafanya maboresho makubwa ya huduma za kifedha kwa wateja wake ili kuendana na mahitaji  ya soko.

Aidha amesema kwamba maboreshao hayo yatasaidia  kukidhi matarajio ya wateja ambapo hivi sasa huduma nyingi za kibenki zinatolewa kidigitali nakusaidia wateja kupata huduma kwa haraka na rahisi zaidi.



"Huduma za ACB VISA CARD zinamrahisishia mteja kufanya miamala mbalimbali kidigitali mfano ;  kutoa pesa kwenye ATM mbalimbali za VISA popote Duniani, na kufanya manunuzi mtandaoni, kufanya malipo kwenye vituo vya mafuta, kwenye migahawa na kwenye maduka makubwa ( Shopping malls & supermarkets) na nyingine nyingi" amesema Silvest.


Bw. Silvest amewashukuru wateja wote kwa kuendelea kuiamini ACB na kufanya biashara kupitia benki hiyo, nakuwaomba Wajasiriamali na Wafanyakazi kutoka taasisi za umma na binafsi kujiunga na benki ya ACB ili kufurahia huduma bora zaidi kwa uharaka, unafuu na usalama.


No comments:

Post a Comment

Pages