HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 13, 2024

RAIS SAMIA AONGOZA KIKAO MAALUM IKULU NDOGO YA TUNGUU ZANZIBAR

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ameongoza kikao maalum kilichowasilisha ripoti ya maafa ya Mafuriko yaliotokea sehemu mbalimbali nchini ikiwemo Rufiji, Morogoro, Lindi na Arusha. Vile vile, kamati maalum imewasilisha maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu ndogo ya Tunguu Zanzibar tarehe 13, Aprili 2024.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alipokuwa akiwasilisha ripoti ya maafa ya Mafuriko yaliotokea sehemu mbalimbali nchini ikiwemo Rufiji, Morogoro, Lindi na Arusha, Ikulu ndogo ya Tunguu Zanzibar tarehe 13, Aprili 2024.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa kikao maalum kilichoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kilichowasilisha ripoti ya maafa ya Mafuriko yaliotokea sehemu mbalimbali nchini ikiwemo Rufiji, Morogoro, Lindi na Arusha pamoja na maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu ndogo ya Tunguu Zanzibar tarehe 13, Aprili 2024.

Baadhi ya Viongozi waliohudhuria kikao maalum kilichoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kilichowasilisha ripoti ya maafa ya Mafuriko yaliotokea sehemu mbalimbali nchini ikiwemo Rufiji, Morogoro, Lindi na Arusha pamoja na wasilisho la Kamati Maalum juu ya maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu ndogo ya Tunguu Zanzibar tarehe 13, Aprili 2024.

No comments:

Post a Comment

Pages