HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 26, 2024

TETESI ZA SOKA MAJUU

Manchester United wana imani dau la kati ya paund milioni 60 mpaka 70 litatosha kumsajili beki wa Uingereza Jarrad Branthwaite (21) kabla ya Juni 30, na hivyo kuiruhusu Everton kujumuisha ada hiyo katika akaunti zao za 2023-24 na kuepuka kukatwa pointi zaidi. (Football Insider)


Vinara wa EPL Arsenal na Manchester City wamefahamishwa kuwa Newcastle United wako tayari kusikiliza ofa zinazozidi thamani ya paund milioni 80 kwa kiungo wa kati wa Brazil Bruno Guimaraes (26) msimu ujao. (90min)


Manchester United wanaweza kuanza kusaka usajili wa beki wa kushoto wa Uhispania Miguel Gutierrez (22) kutoka Girona lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Arsenal na West Ham . (GiveMeSport)


Miamba ya Uholanzi Ajax wana nia ya kumteua meneja wa zamani wa Chelsea na Brighton Graham Potter, ambaye pia yuko kwenye orodha ya Manchester United ya watu wanaoweza kuchukua nafasi ya Erik ten Hag. (Guardian)


Nae Meneja wa zamani wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer na mkufunzi wa zamani wa Leeds United Jesse Marsch wamewasiliana na Canada kuhusu kuiongoza timu ya taifa katika Kombe la Dunia la 2026. (Standard)


Napoli ya Italia wamejiunga na kinyang'anyiro cha kumsajili fowadi wa Canada Jonathan David (24) kutoka Lille . (Calciomercato - in Italian)


Nayo Klabu ya Bundesliga Stuttgart iko tayari kufanya uhamisho wa fowadi wa Ujerumani Deniz Undav, 27, kuwa wa kudumu baada ya kumsajili kwa mkopo kutoka Brighton msimu uliopita wa joto. (Caught Offside)


Habari hizi ni kwa msaada wa mtandao na Tovuti ya bbc.swahili 

No comments:

Post a Comment

Pages