HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 26, 2024

NI MZIZIMA DERBY FAINALI YA MUUNGANO

Na John Marwa


Ndiyoooo, ni Mzizima Derby, fainali ya Kombe la Muungano 2024 katika kuazimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni baada ya ushindi wa mabao 5-2 walioupata Azam FC dhidi ya KMKM, umeifanya timu hiyo kufuzu fainali ya Kombe la Muungano, michuano inayofanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. 



Azam imepata ushindi huo kupitia mabao ya Abdul Sopu dakika ya 7 na 42, huku wafungaji wengine wakiwa ni Nathaniel Chilambo (dk 9), Iddy Seleman (dk 49) na Iddy Kichindo (dk74).



Kwa upande wa mabao ya KMKM yote mawili yalifungwa na Abrahman Ali likiwemo moja kwa mkwaju wa penalti dakika ya 38.


Azam inaungana na Simba kucheza fainali ya michuano hiyo itakayopigwa Jumamosi Aprili 27, 2024 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.


Ikumbukwe kuwa miamba hiyo msimu huu imekutana mara moja na mchezo huo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara NBC PL ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 katika Dimba la Kirumba jijini Mwanza.


No comments:

Post a Comment

Pages