HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 22, 2024

AZIZ KI MTEGONI KWA FEI TOTO

Na John Richard Marwa

Wakati Simba na Azam FC wakipambania nafasi ya pili vita kubwa nyingine kwenye Ligi ni ya ufungaji Bora ni kati ya Feisal Salum Fei Toto dhidi ya Stephanie Aziz Ki.

Hadi muda huu Feisal Salum Fei Toto ameweka kambani mabao 16 huku Aziz Ki akiwa na mabao 15 na akiwa na mchezo mmoja ambapo leo Yanga wanashuka dimbani Jamhuri Dodoma kuwavaa Dodoma Jiji jioni ya leo.

Feisal Salum alifunga bao lake la 16 hapo Jana ambapo Azam walishinda mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania mchezo uliopigwa Dimba la Meja General Isamuhyo.

Kama Aziz Ki leo atafunga basi atamfikia Fei Toto ama kumpita huku kila mmoja akisaliwa na michezo miwili kujulikana nani ni mfungaji bora msimu huu wa 2023/2024.

Swali kuu ni nani kuibuka na kiatu cha ufungaji bora. Ikumbukwe kuwa Yanga wana michezo miwili ukitoa wa leo dhidi ya Dodoma Jiji watacheza na Tabora United Mei 25 kisha wakihitimisha na Tanzania Prisons wakati huo Azam FC watawaalika Kagera Sugar kisha kumfuata Geita Gold FC Mei 28.



No comments:

Post a Comment

Pages