Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay (katikati), Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Prof. Neema Mori
(wapili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid
Nsekela (watatu kushoto), Katibu wa Kampuni Benki ya CRDB, John Rugambo
(watatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully
Esther Mwambapa (wakawanza kushoto, Mkurugenzi wa Manunuzi Benki ya
CRDB, Pendason Philemon (Wakwanza kulia), na Meneja wa Kanda ya
Kaskazini Benki ya CRDB, Cosmas Sadat wakionyesha Taarifa ya Mwaka 2022
ya Benki ya CRDB wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuwakaribisha
wanahisa wa benki hiyo katika Mkutano Mkuu wa 29 utakaofanyika siku ya
jumamosi ya tarehe 18 Mei 2024.
====== ======== =======
Arusha
16 Mei 2024 - Benki ya CRDB inatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa 29 wa
Wanahisa siku ya Jumamosi tarehe Mei 18 kuanzia saa 2 asubuhi katika
Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). Taarifa hiyo
imetolewa leo katika mkutano na waandishi wa habari uuliofanyika hoteli
ya Gran Melia ambapo Benki ya CRDB pia ilizindua Ripoti yake ya Mwaka na
Ripoti ya Uendelevu kwa mwaka 2023.
Mkutano huo unafanyika kufuatana na Sheria ya Makampuni namba 212 ya mwaka 2002, ambapo kila mwaka Benki ya CRDB imekuwa ikiandaa mkutano huo unaowapa Wanahisa fursa ya kujadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupitisha au kuidhinisha maamuzi mbalimbali yenye maslahi kwa Benki.
Akizungumzia
katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hoteli ya
Mount Meru jijini Arusha, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya
CRDB, Dkt. Ally Laay amesema mkutano huo utafanyika kwa njia mseto
“Hybrid Meeting” ili kutoa fursa kwa wanahisa wengi zaidi kushiriki kwa
njia ya kidijitali.
Dkt. Laay alisema kupitia mtandaoni Wanahisa wataweza kujiunga kuanzia saa 2:00 asubuhi kupitia link https://escrowagm.com/crdb/login.aspx au kupitia SimBanking App, ambapo imewekwa sehemu ya ya kujisajili kushiriki Mkutano Mkuu.
“Tumeweka muongozo wa jinsi ya kushiriki mkutano mkuu kwa njia ya mtandao kupitia tovuti yetu ya www.crdbbank.co.tz,
mitandao yetu ya kijamii, lakini pia maelekezo yametumwa kwa ujumbe
mfupi kwa Wanahisa,” alisema Dkt. Laay huku akiwahakikishia kuwa Benki
hiyo vizuri katika kuhakikisha wanashiriki bila chanagamoto yoyote.
Ajenda
mbalimbali zitajadiliwa katika Mkutano Mkuu wa 29 wa Wanahisa wa Benki
ya CRDB ni pamoja na uchaguzi wa wajumbe huru wa bodi, kuteua wakaguzi
wa hesabu, na kujadili na kupokea Taarifa ya Bodi ya Wakurugenzi, na
Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa, pamoja na gawio kwa mwaka 2023 ambapo
pendekezo la gawio la Sh 50 kwa hisa litawasilishwa.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, alisema pendekeo hilo la
ongezeko la gawio kwa hisa linatokana na Benki ya CRDB kuendelea kupata
matokeo mazuri sokoni ambapo mwaka wa fedha ulioisha ilipata faida baada
ya kodi ya Shilingi 423 bilioni ukilinganisha na Shilingi 351 bilioni
mwaka 2022.
Mkutano
Mkuu wa 29 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB utatanguliwa na semina maalum
kwa wanahisa na umma yenye kauli mbiu ya “Ustawi wa Pamoja”
itakayofanyika siku ya Ijumaa tarehe 17/05/2024 kuanzia saa 3 asubuhi
katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).
Dkt.
Laay amesema Semina hiyo ambayo pia itaambatana na maonyesho ya
wanufaika wa programu ya IMBEJU itafunguliwa na Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela
alisema katika mkutano mkuu wa 29 wanahisa wa benki hiyo watapata nafasi
ya kujadili juu ya mwaka mmoja wa utekelezaji mkakati mpya wa biashara
wa muda wa kati wa miaka mitano wa 2023 – 2027.
Nsekela
alitumia fursa hiyo pia kuwahamasisha wanahisa wa Benki ya CRDB
kujitokeza kwa wingi kwani ushiriki wao utaiwezesha Bodi na Menejiment
kupata maoni yao ya namna bora ya kuboresha utendaji wetu.
Akielezea
kauli mbiu ya Mkutano wa mwaka huu wa Wanahisa wa Benki ya CRDB ya
“Ustawi wa Pamoja”, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki
hiyo, Prof. Neema Mori amesema inaelezea namna ambavyo benki hiyo
imedhamiria si tu kutengeneza faida bali pia kuongeza thamani ya
uwekezaji wa wanahisa, kuchangia maendeleo ya wateja, na jamii kwa
ujumla.
No comments:
Post a Comment